Posted By Posted On

Samatta amuogope Watkins? Hebu acheni zenu nyie!

KWA mashabiki wa soka Tanzania, akili haijawakaa sawa tangu Aston Villa ilipomsajili mshambuliaji mpya, Ollie Watkins.  Hofu ni kipenzi chao, Mbwana Samatta, kupoteza nafasi ya kucheza msimu huu na tayari wapo wanaoamini Samatta anapaswa kukimbia na kusaka timu nyingine. Hilo sikubaliani halo. Watkins ametokea Brentford ya Ligi Daraja la Kwanza England (Championship) na ukitazama takwimu,,

KWA mashabiki wa soka Tanzania, akili haijawakaa sawa tangu Aston Villa ilipomsajili mshambuliaji mpya, Ollie Watkins. 

Hofu ni kipenzi chao, Mbwana Samatta, kupoteza nafasi ya kucheza msimu huu na tayari wapo wanaoamini Samatta anapaswa kukimbia na kusaka timu nyingine. Hilo sikubaliani halo.

Watkins ametokea Brentford ya Ligi Daraja la Kwanza England (Championship) na ukitazama takwimu, una kila sababu ya kumpigia saluti. Hilo halina ubishi.

Huko ameacha balaa kwa ubora wake wa kuzipasia nyavu, akimaliza msimu uliopita akiwa amepachika mabao 26. Timu yake, Brentford, ingetia mguu Ligi Kuu kama si kufungwa na Fulham.

Kwa ufupi, Watkins si mchezaji wa kubezwa, hivyo haishangazi kuona Watanzani wakiwa na hofu ya kumuona Samatta akipotezwa kwenye kikosi cha Villa.

Lakini je, mashabiki wa Watkins nao wanamfahamu vyema Samatta? Wanajua ilivyohitaji mapigano ya jasho na damu kupata namba TP Mazembe?

Siibezi TP Mazembe ya sasa bali naizungumzia ile iliyotwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2015 kwa kuwafunga USM Alger.

TP Mazembe ninayotaka uielewe ni ile ya Tresor Mputu akiwa staa kweli kweli. TP Mazembe ya Muteba Kidiaba akiwa kwenye ubora wake langoni, Jean Kasusula, Rainford Kalaba, Stoppila Sunzu, Given Singuluma, na Nathan Sinkala.

Samatta alifika pale, akatulia, akajua changamoto iliyo mbele yake, kisha akajikoki, na hatimaye akawa staa wa timu kama ilivyokuwa kwa Mputu na hao wengine niliowataja.

Je, mashabiki wanaohofia Samatta atapotea wameshasahau ubora wake wa wakati huo? Hawataki tena kukumbuka alivyowika mbele ya akina Mputu kwa kuifungia TP Mazembe bao katika mechi hiyo ya fainali dhidi ya USM Alger?

Kama nilivyotangulia kusema, Watkins ni mshambuliaji mzuri lakini nisishindwe kumwambia ubora wake wa Championship unazidiwa na tuzo ya Mchezaji Bora wa CAF kwa nyota wa Ligi za Ndani aliyoibeba Samatta mwaka 2016.

Nakosa kipimo lakini bado sioni ninavyoweza kushawishika kuwa Championship ni ligi bora kuliko Ligi Kuu ya Ubelgiji, ambayo kwa msimu uliopita Samatta aliwika mara mbili; mfungaji bora na mchezaji bora wa Afrika kwenye ligi hiyo.

Wakati huo huo, najaribu kupima ukomavu wa Watkins na Samatta na hapo nabaini udhaifu mdogo wa Muingereza huyo mbele ya nahodha wetu kwenye kikosi cha Taifa Stars.

Hivi, Samatta aliyecheza michuano mikubwa ya Ulaya, Ligi ya Mabingwa na Ligi ya Europa, tena akikutana na vigogo, ikiwamo Liverpool aliyotikisa nyavu zao, ana cha kuhofia mbele ya mchezaji anayecheza Ligi Kuu kwa mara ya kwanza katika historia ya maisha yake?

Ni kwa maana hiyo basi, kuna aina mbili ya kumzungumzia Watkins mbele ya Samatta. Mosi, tunaweza kuwaita wote kuwa ni wachezaji wa daraja la juu, kwamba Mzungu huyo asionekana bora na tishio zaidi mbele ya Samatta.

Au, tukubaliane na takwimu zilizopo, zikionesha kuWA Watkins aliyetokea ‘mchangani’ ana safari ndefu kufika levo za kueza Ligi ya Mabingwa au Ligi ya Europa kama alivyofanya mtoto wa Tandale.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *