Posted By Posted On

SIMBA KUSHUKA UWANJANI KESHO KUMENYANA NA AFRICAN LYON

 KIKOSI cha Simba kesho, Septemba 21 kinatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya African Lyon inayoshiriki Ligi daraja la Kwanza kwa ajili ya kuwapa nafasi wachezaji ambao hawajacheza mechi za ushindani kuwa fiti.Pia mchezo huo ni maalumu kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa ligi dhidi ya Gwambina FC ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.Mchezo huo utapigwa Uwanja wa Azam Complex majira ya saa 10:00 jioni ambapo kiingilio ni buku tatu mzunguko na buku tano kwa VIP. Ofisa Habari wa Simba Haji Manara amesema kuwa mashabiki ni muhimu kujitokeza kuendelea kuipa sapoti timu yao.”Natambua kwamba mashabiki wanaipenda timu yao ndio maana tumeona kwamba viingilio viwe ile kiasi chake kwenye mechi zetu za ligi pia lakini ninawaomba mjitokeze kwa wingi  kuipa sapoti timu yenu.”Malengo ya mchezo huu ni kwa ajili ya kuwapa uimara wachezaji wetu hasa wale ambao walikosa kucheza mechi za hivi karibuni ili kwenda sawa na kasi ya ushindani.”Huu ni mpango wa Kocha Mkuu, (Sven Vandenbroeck) katika kuimarisha kikosi hivyo mashabiki endeleeni kuipa sapoti timu bila kuchoka,” amesema. Baada ya jana Septemba 20 kumalizana na Biashara United kwa ushindi wa mabao 4-0 mchezo wa Simba unaofuata ni Septemba 26 Uwanja wa Mkapa dhidi ya Gwambina FC.,


 KIKOSI cha Simba kesho, Septemba 21 kinatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya African Lyon inayoshiriki Ligi daraja la Kwanza kwa ajili ya kuwapa nafasi wachezaji ambao hawajacheza mechi za ushindani kuwa fiti.


Pia mchezo huo ni maalumu kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa ligi dhidi ya Gwambina FC ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.


Mchezo huo utapigwa Uwanja wa Azam Complex majira ya saa 10:00 jioni ambapo kiingilio ni buku tatu mzunguko na buku tano kwa VIP. Ofisa Habari wa Simba Haji Manara amesema kuwa mashabiki ni muhimu kujitokeza kuendelea kuipa sapoti timu yao.


“Natambua kwamba mashabiki wanaipenda timu yao ndio maana tumeona kwamba viingilio viwe ile kiasi chake kwenye mechi zetu za ligi pia lakini ninawaomba mjitokeze kwa wingi  kuipa sapoti timu yenu.


“Malengo ya mchezo huu ni kwa ajili ya kuwapa uimara wachezaji wetu hasa wale ambao walikosa kucheza mechi za hivi karibuni ili kwenda sawa na kasi ya ushindani.


“Huu ni mpango wa Kocha Mkuu, (Sven Vandenbroeck) katika kuimarisha kikosi hivyo mashabiki endeleeni kuipa sapoti timu bila kuchoka,” amesema. 


Baada ya jana Septemba 20 kumalizana na Biashara United kwa ushindi wa mabao 4-0 mchezo wa Simba unaofuata ni Septemba 26 Uwanja wa Mkapa dhidi ya Gwambina FC.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *