Posted By Posted On

Sven ashindwa kuvunja rekodi Simba

ZAINAB IDDY KOCHA wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameshindwa kuvunja rekodi iliyoachwa na mwenzake aliyemtangulia Patrick Aussems katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu. Sven amejiunga na  Klabu ya Simba Desemba mwaka jana,  akichukua mikoba ya Aussems, ambaye katika michezo miwili ya msimu huu, amevuna pointi nne huku timu yake ikifunga mabao matatu na kufungwa mawili.,

ZAINAB IDDY

KOCHA wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameshindwa kuvunja rekodi iliyoachwa na mwenzake aliyemtangulia Patrick Aussems katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Sven amejiunga na  Klabu ya Simba Desemba mwaka jana,  akichukua mikoba ya Aussems, ambaye katika michezo miwili ya msimu huu, amevuna pointi nne huku timu yake ikifunga mabao matatu na kufungwa mawili.

Matokeo hayo ya timu hiyo, yanaonekana  kushindwa kuifikia rekodi ya Aussems aliyeweza kuvuna pointi sita katika michezo miwili ya mwanzo wa msimu uliopita, kabla ya ujio wake.

Katika michezo hiyo miwili chini ya Aussems, Simba ilifunga mabao matano na kufungwa mabao mawili, ambapo ilianza kwa ushindi wa 3-1 dhidi ya JKT Tanzania, kisha ushindi wa 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar.

Msimu huu, timu ya Simba ilianza kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ihefu katika mchezo uliochezwa Septemba 7, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya.

Baada ya mchezo huo, timu ya Simba ilitoka sare ya bao 1-1 na Mtibwa Sugar uliochezwa hivi karibuni kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *