Posted By Posted On

TUSIZOEANE

ASHA KIGUNDULA TUSIZOEANE! Unaweza kusema hivyo, baada ya Simba kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Biashara United katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Biashara United uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam. Katika mchezo huo wa jana, ambao ni wa kwanza kwa Simba wakiwa nyumbani, baada ya kuifunga,

ASHA KIGUNDULA

TUSIZOEANE! Unaweza kusema hivyo, baada ya Simba kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Biashara United katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Biashara United uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo wa jana, ambao ni wa kwanza kwa Simba wakiwa nyumbani, baada ya kuifunga Ihefu mabao 2-1 mkoani Mbeya, kisha sare ya bao 1-1 na Mtibwa Sugar mjini Morogoro,  ulichezeshwa na mwamuzi Abel William kutoka Arusha.

Simba walianza mchezo huo kwa kasi na kufanikiwa kupata mabao yaliyofungwa na Clatous Chama aliyetupia mawili, Middie Kagere na Chris Mugalu.

Wekundu wa Msimbazi walianza kulishambulia lango la Biashara United dakika ya kwanza, ambapo kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Larry Bwalya alikosa bao baada ya kupiga shuti hafifu na mpira kutoka nje ya lango la wapinzani wao.

Chama alifunga bao la kuongoza dakika ya tisa baada ya kumalizia kazi nzuri ya Luis Miquissone.

Katika dakika ya 18, mwamuzi William alimwonesha kadi ya njano mchezaji wa Biashara United, Ally Mussa, baada ya kumchezea rafu kiungo mshambuliaji wa Simba, Mzamiru Yassin.

Dakika ya 26, Chama aliwainua kwa mara nyingine mashabiki wa Simba baada ya kuongeza bao la pili akimalizia krosi safi ya Luis aliyeng’ara katika mchezo huo. 

Hata hivyo, Biashara United walipoteza nafasi ya wazi ya kufunga dakika ya 27, baada ya Abdumajid Mangaro kupiga shuti lililookolewa na kipa wa Simba, Manula.

Biashara United walipoteza nafasi nyingine ya kufunga dakika ya 38, baada ya Lenny Vedastus  kupiga shuti la mbali na mpira kutoka nje.

Kegere alianza kusaka kiatu cha dhahabu baada ya kufunga bao la tatu dakika ya 52 kwa shuti kali huku akimwacha kipa wa Biashara United, Daniel Mgore, akigaagaa bila mafanikio.

Mwamuzi William alimwonesha kadi ya njano mchezaji wa Biashara United, Omar Hassan dakika ya 60 baada ya kumchezea rafu Luis.

Mugalu aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Kagere alikosa bao la wazi dakika ya 80, baada ya kushindwa kumalizia pasi ya mwisho ya Bernard Morrison. 

Hata hivyo, Mugalu alisahihisha makosa yake dakika nne baadaye, baada ya kuifungia Simba bao la nne, kutokana na shambulizi lililoanzia kwa Chama, kisha Morrison, kabla ya mpira kumkuta mfungaji huyo raia wa DR Congo.

Simba; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Joash Onyango, Pascal  Wawa, Gerson Fraga/Hamis Ndemla (dk.16), Luis Miquissone, Mzamiru Yassin, Middie Kagere/Chris Mugalu (dk.76), Larry Bwalya/ Bernard Morrison  na Clatous Chama.

Biashara United; Daniel Mgore, Ally Mussa/Omar Hassan (dk.20)/Ramadhan Chombo, Deogratius Judika,
Tariq Simba, Kelvin Friday/Gerson Samwel (dk.79),  Mpapi Nasib,
Mustapha Khamis,  Lenny Vedastus,  Abdulmajid  Mangaro na Omary Abdallah/Gerald Mathias (dk.63).

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *