Posted By Posted On

United ‘kimeo’ yamtoa povu Evra

MANCHESTER, England BEKI wa zamani wa Manchester United, Patrice Evra, amekerwa na namna mambo yanayoendelea katika klabu hiyo, hasa ishu za usajili. Evra alisikitishwa na kiwango kibovu kilichooneshwa na Man United  juzi na kusababisha ichapwe mabao 3-1 na Crystal Palace. “Kuna mapungufu mengi sana Man United na sisemi hivyo kwa sababu tumefungwa.  Ukiangalia usajili, unasuasua,

MANCHESTER, England

BEKI wa zamani wa Manchester United, Patrice Evra, amekerwa na namna mambo yanayoendelea katika klabu hiyo, hasa ishu za usajili.

Evra alisikitishwa na kiwango kibovu kilichooneshwa na Man United  juzi na kusababisha ichapwe mabao 3-1 na Crystal Palace.

“Kuna mapungufu mengi sana Man United na sisemi hivyo kwa sababu tumefungwa.  Ukiangalia usajili, unasuasua sana. Kwa kweli inachosha na kuumiza…” alisema Evra.

Evra, beki wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa, aliyasema hayo kupitia kituo cha televisheni cha Sky Sports.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *