Posted By Posted On

WALIOIMALIZA MBEYA CITY JANA LEO WAWEKWA KANDO NDANI YA AZAM FC

 KOCHA Msaidizi wa Azam FC Vivier Bahati amesema kuwa wachezaji wake walioanza kikosi cha kwanza jana mbele ya Mbeya City leo walipata muda wa kupumzika kabla ya kuanza kujumuika na wengine kesho kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao ujao dhidi ya Tanzania Prisons.Azam FC ilishinda kwa bao 1-0 mbele ya Mbeya City, Uwanja wa Sokoine bao lililopachikwa na Ally Niyonzima dakika ya 23 kwa pasi ya Nivere Tigere.Wengine ambao walianza kikosi cha kwanza Septemba 20 ni pamoja na David Kissu, Prince Dube, Nico Wadada, Sure Boy.Bahati amesema:”Wachezaji wote walioanza kikosi cha kwanza mbele ya Mbeya City wamepewa muda wa kupumzika kwanza ili kujiweka sawa kwa kuwa jana walifanya kazi kubwa uwanjani.”Kesho tutaanza mazoezi ya pamoja na wachezaji wengine wote ambao walianza na wale ambao hawakuanza. Tumeanza na hawa ambao hawakuwa kwenye kikosi cha kwanza kwa kuwa tunahitaji nao pia wawe kwenye ubora wao.”Azam FC inajipanga kwenda kumenyana na Tanzania Prisons, Uwanja wa Nelson Mandela,Septemba 26 ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi tisa kibindoni na imefunga mabao manne.,

 


KOCHA Msaidizi wa Azam FC Vivier Bahati amesema kuwa wachezaji wake walioanza kikosi cha kwanza jana mbele ya Mbeya City leo walipata muda wa kupumzika kabla ya kuanza kujumuika na wengine kesho kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao ujao dhidi ya Tanzania Prisons.

Azam FC ilishinda kwa bao 1-0 mbele ya Mbeya City, Uwanja wa Sokoine bao lililopachikwa na Ally Niyonzima dakika ya 23 kwa pasi ya Nivere Tigere.


Wengine ambao walianza kikosi cha kwanza Septemba 20 ni pamoja na David Kissu, Prince Dube, Nico Wadada, Sure Boy.

Bahati amesema:”Wachezaji wote walioanza kikosi cha kwanza mbele ya Mbeya City wamepewa muda wa kupumzika kwanza ili kujiweka sawa kwa kuwa jana walifanya kazi kubwa uwanjani.


“Kesho tutaanza mazoezi ya pamoja na wachezaji wengine wote ambao walianza na wale ambao hawakuanza. Tumeanza na hawa ambao hawakuwa kwenye kikosi cha kwanza kwa kuwa tunahitaji nao pia wawe kwenye ubora wao.”


Azam FC inajipanga kwenda kumenyana na Tanzania Prisons, Uwanja wa Nelson Mandela,Septemba 26 ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi tisa kibindoni na imefunga mabao manne.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *