Posted By Posted On

ZLATKO AWATOA HOFU WANAYANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Kocha Mkuu wa Yanga, Zlatko Krmpotic amewashusha presha mashabiki wa timu akiwaambia mabao yatakuja, kwani kilichomuhimu kwake kwanza ni kuvuna alama tatu muhimu ili kujiweka pazuri na kusema wapinzani wao watapata tabu sana juu yao.

Yanga katika mechi zao tatu za awali za Ligi Kuu Bara mpaka sasa imefunga mabao matatu, huku nikiruhusu moja na kutowapa furaha mashabiki wao kutokana na majembe iliyonayo kikosini, lakini Kocha Zlatko amewatuliza akiwaaambia anaijenga kwanza timu.

Akizungumza jana mara baada ya kurejea jijini Dar es Salaam wakitokea Bukoba walipowachapa Kagera Sugar kwa bao 1-0, kocha huyo alisema hata yeye hakubaliani na kasi ndogo ya ufungaji mabao kwa ubora wa kikosi chake, lakini anajua mambo yanajengwa taratibu na Yanga itatisha.

Kocha Zlatko alisema bado anataka kuona kikosi chake kinatumia zaidi nafasi wanazotengeneza uwanjani, lakini timu inaposhinda ni hatua muhimu kwa kuwa sio rahisi kupata matokeo.

“Siwezi kuridhika na kila kitu, lakini nafurahi kuona timu inashinda kwa sasa tukiwa nyumbani na hata ugenini. Sio rahisi lakini narudia hapa bado tunatengeneza timu mambo mazuri hayawezi kuja kwa haraka sana,” alisema Zlatko

“Kuna wakati tunatakiwa tutumie zaidi nafasi tunazotengeneza katika mechi, angalia jana (juzi) kuna nafasi ya uhakika Carlinhos (Carlos Fernandez) aliipoteza hili sio zuri, lakini bado kuna kazi tunatakiwa kuifanya na wapinzani wetu wajiandae kupata tabu ikiimarika zaidi.

Aidha kocha huyo kwa sasa wanaingia katika maandalizi ya mchezo unaofuatia dhidi ya Mtibwa Sugar, akidai Ligi Kuu Bara, hakuna mechi rahisi kutokana na wapinzani wao nao wanajiandaa vyema kuhakikisha wanawazuia lakini anafurahi kuona morali ya nyota wake ipo juu.

“Nafurahia kuona wachezaji wangu sio watu wanaokata tamaa,nidhamu yao ya kupambana ipo juu sana narudia kusema hii ni timu mpya kuna mambo yatakuwa sawa taratibu hatujacheza mechi rahisi mpaka sasa kila mechi ina ugumu wake.”

,,Read More

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *