Posted By Posted On

Azam FC yakiri Mbeya City kiboko

NA WINFRIDA MTOI LICHA ya kuchukua alama tatu kwa Mbeya City, uongozi wa Azam FC umekiri haikuwa kazi rahisi kutokana na soka walilocheza wapinzani wao. Azam juzi ilifanikiwa kushinda bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya. Akizungumza na BINGWA kutoka jijini Mbeya jana, Mkuu wa Kitengo cha,

NA WINFRIDA MTOI

LICHA ya kuchukua alama tatu kwa Mbeya City, uongozi wa Azam FC umekiri haikuwa kazi rahisi kutokana na soka walilocheza wapinzani wao.

Azam juzi ilifanikiwa kushinda bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Akizungumza na BINGWA kutoka jijini Mbeya jana, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Azam, Thabit Zakaria, alisema mchezo ulikuwa mgumu kwa sababu Mbeya City walikuwa wanawashambulia kila mara.

Alisema wapinzani wao walikuwa wanacheza mpira wa nguvu kutokana na kuzoea uwanja huo, hali iliyowapa wakati mgumu katika kutafuta pointi tatu.

β€œUkweli mchezo ulikuwa mgumu, Mbeya City wametushambulia sana, wazuri katika utimamu wa mwili na kutumia nguvu, pia walicheza mipira mirefu ambayo ilitupa shida,” alisema.

Alisema muhimu ni alama tatu walizopata na wanaanza maandalizi ya mchezo ujao dhidi ya Tanzania Prisons utakaochezwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Mandela, Sumbawanga.

Ushindi huo umeifanya Azam kufikisha alama tisa katika michezo mitatu waliyocheza na haijaruhusu lango lao kutikiswa.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *