Posted By Posted On

AZAM FC YATAKA KUENDELEZA REKODI YAKE

 UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa hesabu zao kubwa ni kuendeleza rekodi zao ndani ya Ligi Kuu Bara ili kufikia malengo ambayo wamejiwekea.Azam FC kwenye msimamo ipo nafasi ya pili ikiwa imecheza mechi tatu ambazo ni dakika 270 na haijapoteza mchezo kibindoni ina poiti tisa.Kwenye mechi zake tatu ilizocheza safu yake ya ushambuliaji inayoongozwa na Obrey Chirwa ambaye msimu uliopita alisepa na mipira miwili baada ya kufunga ‘hattrick’ mbili msimu huu wa 2020/21 imefunga jumla ya mabao manne na safu ya ulinzi inayoongozwa na Nicolas Wadada haijaruhusu bao.Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa kila kitu kinakwenda sawa kutokana na mipango mizuri iliyowekwa ili kuendeleza rekodi yao.”Tumeanza vizuri kwetu ni jambo la kumshukuru Mungu lakini malengo yetu makubwa ni kuona kwamba rekodi yetu ya kushinda inaendelea kwenye mechi zetu zote,” amesema.Ilianza kushinda bao 1-0 mbele ya Polisi Tanzania kisha ikaibuka na ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Coastal Union zote zilipigwa Uwanja wa Azam Complex kabla ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Mbeya City Uwanja wa Sokoine.,


 UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa hesabu zao kubwa ni kuendeleza rekodi zao ndani ya Ligi Kuu Bara ili kufikia malengo ambayo wamejiwekea.


Azam FC kwenye msimamo ipo nafasi ya pili ikiwa imecheza mechi tatu ambazo ni dakika 270 na haijapoteza mchezo kibindoni ina poiti tisa.


Kwenye mechi zake tatu ilizocheza safu yake ya ushambuliaji inayoongozwa na Obrey Chirwa ambaye msimu uliopita alisepa na mipira miwili baada ya kufunga ‘hattrick’ mbili msimu huu wa 2020/21 imefunga jumla ya mabao manne na safu ya ulinzi inayoongozwa na Nicolas Wadada haijaruhusu bao.


Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa kila kitu kinakwenda sawa kutokana na mipango mizuri iliyowekwa ili kuendeleza rekodi yao.


“Tumeanza vizuri kwetu ni jambo la kumshukuru Mungu lakini malengo yetu makubwa ni kuona kwamba rekodi yetu ya kushinda inaendelea kwenye mechi zetu zote,” amesema.


Ilianza kushinda bao 1-0 mbele ya Polisi Tanzania kisha ikaibuka na ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Coastal Union zote zilipigwa Uwanja wa Azam Complex kabla ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Mbeya City Uwanja wa Sokoine.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *