Posted By Posted On

FT:SIMBA 2-0 AFRICAN LYON

 Mchezo wa kirafiki kati ya Simba na African Lyon uliochezwa leo Septemba 22 Uwanja wa Azam Complex umekamilika kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.Mabao ya Simba  yalipachikwa kimiani na Chris Mugalu dakika ya 46 kwa pasi ya Ibrahim Ajibu na bao la pili lilipachikwa kimiani na Charlse Ilanfya dakika ya 53 kwa pasi ya Gadiel Michael.Kwenye mchezo wa leo mashabiki walijitokeza wengi kipindi cha pili baada ya mpira kuanza kipindi cha kwanza ukiwa na mashabiki wachache kiasi chake.Dakika 45 za kwanza timu zote zilitoshana nguvu na kuwafanya Simba pamoja African Lyon kwenda vyumba vya kubadilishia nguo wakiwa hawajafungana ila mambo yote yalibadilika kipindi cha pili.African Lyon ipo kwenye maandalizi ya kujiaandaa kwa ajili ya kushiriki Ligi Daraja la Kwanza ikiwa ipo kundi A huku Simba ikijiandaa na mechi za Ligi Kuu Bara.,

 


Mchezo wa kirafiki kati ya Simba na African Lyon uliochezwa leo Septemba 22 Uwanja wa Azam Complex umekamilika kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.


Mabao ya Simba  yalipachikwa kimiani na Chris Mugalu dakika ya 46 kwa pasi ya Ibrahim Ajibu na bao la pili lilipachikwa kimiani na Charlse Ilanfya dakika ya 53 kwa pasi ya Gadiel Michael.

Kwenye mchezo wa leo mashabiki walijitokeza wengi kipindi cha pili baada ya mpira kuanza kipindi cha kwanza ukiwa na mashabiki wachache kiasi chake.

Dakika 45 za kwanza timu zote zilitoshana nguvu na kuwafanya Simba pamoja African Lyon kwenda vyumba vya kubadilishia nguo wakiwa hawajafungana ila mambo yote yalibadilika kipindi cha pili.

African Lyon ipo kwenye maandalizi ya kujiaandaa kwa ajili ya kushiriki Ligi Daraja la Kwanza ikiwa ipo kundi A huku Simba ikijiandaa na mechi za Ligi Kuu Bara.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *