Posted By Posted On

KISINDA AAHIDI MAMBO MAZURI YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Winga wa Yanga, Tuisila Kisinda anasema hakuna mchezo uliomnyima raha kama wa Mbeya City na kwamba kitendo cha kujiangusha hovyo kilimpunguzia kasi akitaka timu zipambane kutafuta matokeo.

“Ni vyema timu zote zikapambana uwanjani, sipendi kuona wachezaji wanaanguka wanapoteza muda, ushindani upo wapi, wachezaji wanajituma lakini wale wanaopoteza muda hawafanyi kitu kizuri kabisa,” alisema Kisinda.

“Kila mchezaji anatakiwa kujituma uwanjani aisaidie timu yake kupata matokeo, hiyo ndio hatua ninayoitaka inakufanya hata wewe uongeze akili na maarifa kuipa matokeo inayotaka.”

Mkongomani huyo alisema kuwa hata kama mashabiki wa timu yake wanafurahia uwezo wake, lakini bado hajacheza katika kiwango anachokifahamu.

“Sasa nataka kuwasoma mabeki wa timu pinzani, zaidi bado sijacheza katika kiwango changu ninachokijua, kuna mambo najifunza kwanza hapa juu ya timu pinzani kuna wakati watu watafurahi zaidi,” alisema.

“Tuna timu bora sana ambayo naamini tunaweza kufanya mambo mazuri kama tutaendelea kuwa wamoja na kuipigania timu yetu, lakini hatua nzuri zaidi mashabiki wetu wanatuhamasisha kujituma uwanjani.

“Hapa Tanzania watu wanapenda sana mpira, nafurahi kuona mashabiki wanasafiri na timu kila inapokwenda na wanataka matokeo, hii inakupa hamasa kwamba mchezaji unatakiwa kujituma uwanjani ili nao wafurahi.”

,,Read More

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *