Posted By Posted On

LIVERPOOL IPO KWENYE HESABU ZA KUPATA SAINI YA MBAPPE

IMERIPOTIWA kuwa Klabu ya Liverpool ipo kwenye hesabu za kumpata mshambuliaji wa Klabu ya Paris Saint-German,(PSG) Kylian Mbappe kwa ajili ya kuibukia ndani ya kikosi hicho ambacho kinatetea taji la Ligi Kuu England.Saini ya Mbappe raia wa Ufaransa pia inawindwa na Klabu ya Real Madrid jambo ambalo linaongeza ushindani kwa timu hizi mbili kubwa kupambana kupata saini yake.Mbappe mkataba wake ndani ya PSG bado unaishi kwa kuwa amebakiza dili la miaka miwili lakini kuna kipengele cha kufanya makubaliano na timu ambayo inahitaji saini yake.Kwa mujibu wa gazeti moja la nchini Ufaransa la L’Equipe limeripoti kuwa Kocha Mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp anamtazama kwa ukaribu Mbappe ili kumuongeza ndani ya kikosi chake na kumtoa ndani ya Ligue 1  ili ashiriki Ligi Kuu England.,


IMERIPOTIWA kuwa Klabu ya Liverpool ipo kwenye hesabu za kumpata mshambuliaji wa Klabu ya Paris Saint-German,(PSG) Kylian Mbappe kwa ajili ya kuibukia ndani ya kikosi hicho ambacho kinatetea taji la Ligi Kuu England.


Saini ya Mbappe raia wa Ufaransa pia inawindwa na Klabu ya Real Madrid jambo ambalo linaongeza ushindani kwa timu hizi mbili kubwa kupambana kupata saini yake.

Mbappe mkataba wake ndani ya PSG bado unaishi kwa kuwa amebakiza dili la miaka miwili lakini kuna kipengele cha kufanya makubaliano na timu ambayo inahitaji saini yake.

Kwa mujibu wa gazeti moja la nchini Ufaransa la L’Equipe limeripoti kuwa Kocha Mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp anamtazama kwa ukaribu Mbappe ili kumuongeza ndani ya kikosi chake na kumtoa ndani ya Ligue 1  ili ashiriki Ligi Kuu England.


,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *