Posted By Posted On

MTIBWA SUGAR WAIPA SOMO KIMTINDO SIMBA KUHUSU WACHEZAJI WA GHARAMA

OFISA Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amefichua kuwa kabla ya matokeo ya sare na Simba, wapinzani wao walijuwa watawafunga zaidi ya mabao 10 kutokana na uwepo wa wachezaji waliowasajili kwa gharama akiwemo Bernard Morrison na Larry Bwalya.Kifaru ameongeza kuwa kwa aina ya wachezaji ambao Simba wamewasajili kwa gharama kubwa wengi walijuwa wangepoteza mechi hiyo na Simba kwa idadi kubwa ya mabao.Mtibwa wakiwa kwenye Uwanja wao wa nyumbani wa Jamhuri, Morogoro waliwalazimisha Simba sare ya kufungana bao 1-1 ilikuwa ni Septemba 12.Kifaru amesema kuwa: “Simba wamesajili kwa gharama kubwa sana, wengi walidhani kwamba watakuwa na uwezo wa kutufunga mabao mengi hata 10.”Lakini wameona kuwa hizo fedha wangeweza kuwapa tu wachezaji wa hapa ndani kisha wakaifanya kazi yao vizuri kama ambavyo sisi tumefanya na kupata matokeo dhidi yao,” aliweka nukta Kifaru.Bao la Simba lilifungwa na Mzamiru Yassin huku lile la Mtibwa Sugar likiwekwa kimiani na nyota wao Boban Zirintusa na kuwafanya wagawane pointi mojamoja.,

OFISA Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amefichua kuwa kabla ya matokeo ya sare na Simba, wapinzani wao walijuwa watawafunga zaidi ya mabao 10 kutokana na uwepo wa wachezaji waliowasajili kwa gharama akiwemo Bernard Morrison na Larry Bwalya.


Kifaru ameongeza kuwa kwa aina ya wachezaji ambao Simba wamewasajili kwa gharama kubwa wengi walijuwa wangepoteza mechi hiyo na Simba kwa idadi kubwa ya mabao.

Mtibwa wakiwa kwenye Uwanja wao wa nyumbani wa Jamhuri, Morogoro waliwalazimisha Simba sare ya kufungana bao 1-1 ilikuwa ni Septemba 12.

Kifaru amesema kuwa: “Simba wamesajili kwa gharama kubwa sana, wengi walidhani kwamba watakuwa na uwezo wa kutufunga mabao mengi hata 10.
“Lakini wameona kuwa hizo fedha wangeweza kuwapa tu wachezaji wa hapa ndani kisha wakaifanya kazi yao vizuri kama ambavyo sisi tumefanya na kupata matokeo dhidi yao,” aliweka nukta Kifaru.

Bao la Simba lilifungwa na Mzamiru Yassin huku lile la Mtibwa Sugar likiwekwa kimiani na nyota wao Boban Zirintusa na kuwafanya wagawane pointi mojamoja.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *