Posted By Posted On

Niyonzima ala kiapo mechi za ugenini

NA ZAINAB IDDY NAHODHA msaidizi wa Yanga, Haruna Niyonzima, amesema kuwa mipango ya timu yao ni kuwa na mwendelezo wa kuvuna alama tatu katika mechi zote za ugenini za Ligi Kuu Tanzania Bara. Kikosi cha Yanga jana mchana kilikutana makao makuu ya klabu hiyo, Mtaa wa Jangwani, Dar es Salaam na kuingia kambini kujiandaa na,

NA ZAINAB IDDY

NAHODHA msaidizi wa Yanga, Haruna Niyonzima, amesema kuwa mipango ya timu yao ni kuwa na mwendelezo wa kuvuna alama tatu katika mechi zote za ugenini za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kikosi cha Yanga jana mchana kilikutana makao makuu ya klabu hiyo, Mtaa wa Jangwani, Dar es Salaam na kuingia kambini kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar watakaocheza Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, Jumapili.

Timu hiyo iliyo chini ya kocha, Zlatko Krmpotic, itakwenda mkoani Morogoro katika mchezo wake wa pili ugenini baada ya awali kukipiga na Kagera Sugar, mjini Bukoba, Kagera na kutoka na ushindi wa bao 1-0.

Niyonzima ameliambia BINGWA jana kuwa Yanga inawaheshimu Mtibwa Sugar, lakini hawatakuwa tayari kuziacha pointi zote tatu katika himaya yao.

“Mtibwa ni timu nzuri sana na inapoamua jambo lake, lazima walitimize, tunajua wanahitaji nao pointi ambazo Yanga tunazitaka, hatuwezi kuwaachia.

“Mipango yetu ni kuvuna alama zote ugenini bila ya kujali tunacheza na timu ipi au uwanja gani tunatumia, tutakwenda kupambana na kurejea nyumbani tukiwa na kile tunachohitaji,” alisema.

Wanajangwani wamecheza mechi tatu hadi sasa, wakishinda mbili na kupata sare mmoja, hivyo kujikusanyia pointi saba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *