Posted By Posted On

SIMBA KUSHUSHA MUZIKI WA KAZI MBELE YA AFRICAN LYON LEO

UONGOZI wa Simba umesema kuwa leo utashusha kikosi kizima cha kazi kwa ajili ya kushinda na kutoa burudani mbele ya African Lyon kwenye mchezo wa kirafiki utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex, majira ya saa 10:00 jioni.Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kila kitu kipo sawa na wamejipanga kuendelea kutoa burudani na kushinda mchezo wao mbele ya African Lyon.”Kawaida ya Simba ni moja siku zote kucheza mpira mzuri ambao utatoa burudani na matokeo chanya kwenye mchezo wetu ambao tunacheza bila kujali ni aina gani ya mchezo.”Hii ni njia bora kwetu itakayotufanya tuwe bora na kwenye mchezo wetu dhidi ya African Lyon ni mahususi kwa ajili ya wale wachezaji ambao hawajapata nafasi ya kucheza muda mrefu pamoja na kuendelea kuifanya timu kuwa bora.”Mashabiki wajitokeze kwa wingi kwa kuwa kiingilio ni cha kawaida sana na tunazidi kuwashukuru kwa kuwa wamekuwa wakitupa sapoti mara kwa mara hivyo wasichoke katika hili,” amesema.Miongoni mwa nyota wa Simba ambao hawajapata muda mwingi wa kucheza ndani ya Simba ni pamoja na Chris Mugalu, Rarry Bwalya, Meddie Kagere, Ibrahim Ajibu na Beno Kakolanya.,

UONGOZI wa Simba umesema kuwa leo utashusha kikosi kizima cha kazi kwa ajili ya kushinda na kutoa burudani mbele ya African Lyon kwenye mchezo wa kirafiki utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex, majira ya saa 10:00 jioni.


Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kila kitu kipo sawa na wamejipanga kuendelea kutoa burudani na kushinda mchezo wao mbele ya African Lyon.

“Kawaida ya Simba ni moja siku zote kucheza mpira mzuri ambao utatoa burudani na matokeo chanya kwenye mchezo wetu ambao tunacheza bila kujali ni aina gani ya mchezo.

“Hii ni njia bora kwetu itakayotufanya tuwe bora na kwenye mchezo wetu dhidi ya African Lyon ni mahususi kwa ajili ya wale wachezaji ambao hawajapata nafasi ya kucheza muda mrefu pamoja na kuendelea kuifanya timu kuwa bora.

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kwa kuwa kiingilio ni cha kawaida sana na tunazidi kuwashukuru kwa kuwa wamekuwa wakitupa sapoti mara kwa mara hivyo wasichoke katika hili,” amesema.

Miongoni mwa nyota wa Simba ambao hawajapata muda mwingi wa kucheza ndani ya Simba ni pamoja na Chris Mugalu, Rarry Bwalya, Meddie Kagere, Ibrahim Ajibu na Beno Kakolanya.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *