Posted By Posted On

YANGA YAZITAKA POINTI TATU ZA MTIBWA SUGAR

 BEKI kisiki wa Yanga, Lamine Moro amesema kuwa wachezaji wapo tayari kwa ajili ya ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara kutokana na maandalizi ambayo wanayafanya.Kwa sasa Yanga inafanya maandalizi kwa ajili ya mchezo wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar unaotarajiwa kuchezwa Septemba 27 Uwanja wa Jamhuri, Morogoro. Kwenye msimamo, Yanga ipo nafasi ya tano baada ya kucheza mechi tatu ikiwa na pointi saba imefunga mabao mawili na kufungwa bao moja inakutana na Mtibwa Sugar iliyo nafasi ya saba na pointi zake tano kibindoni.Moro amesema:”Tunafanya vizuri kutokana na ushirikiano ambao tunao kwa sasa na kila mchezaji anafikiria kuona namna gani timu itapata matokeo.”Ninaamini kwamba kazi haitakuwa rahisi lakini kikubwa ni kuendelea kupambana kwa ajili ya kupata pointi tatu kwa kuwa ndicho tunachokihitaji kwenye mechi zetu zote.”Moro ana bao moja kibindoni ambalo alipachika kwenye ushindi wa bao 1-0 mbele ya Mbeya City, Uwanja wa Mkapa.,


 BEKI kisiki wa Yanga, Lamine Moro amesema kuwa wachezaji wapo tayari kwa ajili ya ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara kutokana na maandalizi ambayo wanayafanya.


Kwa sasa Yanga inafanya maandalizi kwa ajili ya mchezo wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar unaotarajiwa kuchezwa Septemba 27 Uwanja wa Jamhuri, Morogoro. 

Kwenye msimamo, Yanga ipo nafasi ya tano baada ya kucheza mechi tatu ikiwa na pointi saba imefunga mabao mawili na kufungwa bao moja inakutana na Mtibwa Sugar iliyo nafasi ya saba na pointi zake tano kibindoni.

Moro amesema:”Tunafanya vizuri kutokana na ushirikiano ambao tunao kwa sasa na kila mchezaji anafikiria kuona namna gani timu itapata matokeo.


“Ninaamini kwamba kazi haitakuwa rahisi lakini kikubwa ni kuendelea kupambana kwa ajili ya kupata pointi tatu kwa kuwa ndicho tunachokihitaji kwenye mechi zetu zote.”

Moro ana bao moja kibindoni ambalo alipachika kwenye ushindi wa bao 1-0 mbele ya Mbeya City, Uwanja wa Mkapa.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *