Posted By Posted On

ZLATKO AANZA KUSUKA YANGA YA MABAO

Msomaji wa Yanganews Blog:Kocha wa Yanga Zlatko Krmpotic amesema haridhishwi na ushindi mwembamba wa timu yake na sasa anatafuta dawa ya mabao mengi kwa kuanzia na mechi ya Mtibwa Sugar. Yanga inatarajiwa kucheza na Mtibwa Sugar ugenini kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro mwishoni mwa wiki hii.

Mabingwa hao wa kihistoria ina pointi saba, wakishinda mechi mbili na sare moja, katika mechi ilizoshinda ilikuwa ni kwa ushindi wa bao moja moja.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Zlatko alisema tayari timu imeshaingia kambini kujiandaa na mechi hiyo inayotarajiwa kuwa kali. Alisema, wanafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Chuo cha Sheria ambapo anaendelea kuwapa wachezaji wake program zitakazowafanya kutafuta ushindi wa mabao mengi.

“Baada ya mechezo na Kagera Sugar tulioshinda bao 1-0 nimeona sijaridhika na mabao kidogo, sasa nafanyia kazi namna ya kupata ushindi wa mabao mengi tukianzia katika mechi ijayo (dhidi ya Mtibwa Sugar),” alisema.

Alisema pamoja na kwamba wachezaji wake wameanza kuonesha mabadiliko ya kuingia kwenye mfumo wake lakini anahitaji kuwapa mbinu mpya.

“Tunapata ushindi lakini bado unakuwa mdogo tunahitaji kupata mabao mengi kwenye kila mechi na hili ni tatizo ambalo natakiwa kuanza kuwatengenezea program itakayowafanya wachezaji wangu kuwa na mbinu ya kufunga mabao mengi,”alisema.

,,Read More

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *