Posted By Posted On

AZAM FC KAMILI GADO KUMALIZANA NA TANZANIA PRISONS

 UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa Septemba 26 Uwanja wa Nelson Mandela,  Sumbawanga. Azam FC itashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kushinda bao 1-0 mbele ya Mbeya City uliochezwa Uwanja wa Sokoine. Bao pekee la ushindi kwa Azam FC lilipachikwa na Ally Niyonzima akimalizia pasi ya Never Tigere kwa kona iliyokutana na kichwa cha Niyonzima. Ofisa Habari wa Azam FC,  Zakaria Thabit amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa pili ugenini.Inakutana na Tanzania Prisons ambayo imetoka kushinda bao 1-0 mbele ya Namungo FC hivyo mchezo unatarajiwa kuwa na ushindani kwa timu zote mbili kusaka pointi tatu.,

 

UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa Septemba 26 Uwanja wa Nelson Mandela,  Sumbawanga. 


Azam FC itashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kushinda bao 1-0 mbele ya Mbeya City uliochezwa Uwanja wa Sokoine. 


Bao pekee la ushindi kwa Azam FC lilipachikwa na Ally Niyonzima akimalizia pasi ya Never Tigere kwa kona iliyokutana na kichwa cha Niyonzima. 


Ofisa Habari wa Azam FC,  Zakaria Thabit amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa pili ugenini.

Inakutana na Tanzania Prisons ambayo imetoka kushinda bao 1-0 mbele ya Namungo FC hivyo mchezo unatarajiwa kuwa na ushindani kwa timu zote mbili kusaka pointi tatu.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *