Posted By Posted On

BIASHARA UNITED: TIMU IKIENDA KICHWAKICHWA KWA SIMBA ITAPIGWA ZAIDI YA 4G

 FRANCIS Baraza, Kocha Mkuu wa Biashara United amesema kuwa kwa msimu wa 2020/21 ikiwa itatokea timu itaingia kichwakichwa kucheza na Klabu ya Simba itaokota mabao mengi nyavuni.Biashara United mchezo wake wa kwanza nje ya Mara, ilikutana na Simba ambapo ilifungwa mabao 4-0 Uwanja wa Mkapa ilikuwa ni Septemba 20.Kichapo hicho ni cha kwanza kwa Biashara United kupokea kwa msimu huu mpya kwa kuwa ilicheza mechi mbili bila kufungwa bao lolote na ngome ya Daniel Mgore kuwa imara kwa muda wa dakika 180.Baraza alianza kumenyana na Gwambina FC Uwanja wa Karume kwa kushinda bao 1-0 kisha ikamaliza safari yake mbele ya Mwadui FC kwa kushinda bao 1-0 kabla ya kuondoka Mara kuifuata Simba.Baraza amesema:”Simba ni timu kubwa ambayo inafanya vizuri katika mechi zake, lakini ikitokea timu ikaingia kichwakichwa inaweza kufungwa mabao zaidi ya yale ambayo sisi tulifungwa.”wachezaji wangu walikwama katika kutegua makosa yao ambayo waliyatega wenyewe na nafasi ambazo walitengeneza walishindwa kutumia hilo linatufanya tuanze kujipanga upya kwa ajili ya mechi zetu zijazo.”Bado kwa sasa ligi inaanza tuna nafasi ya kufanya vizuri hakuna haja ya kukata tamaa imani yangu ipo kwa wachezaji na nguvu ya kufanya vizuri ipo,” amesema.,


 FRANCIS Baraza, Kocha Mkuu wa Biashara United amesema kuwa kwa msimu wa 2020/21 ikiwa itatokea timu itaingia kichwakichwa kucheza na Klabu ya Simba itaokota mabao mengi nyavuni.

Biashara United mchezo wake wa kwanza nje ya Mara, ilikutana na Simba ambapo ilifungwa mabao 4-0 Uwanja wa Mkapa ilikuwa ni Septemba 20.

Kichapo hicho ni cha kwanza kwa Biashara United kupokea kwa msimu huu mpya kwa kuwa ilicheza mechi mbili bila kufungwa bao lolote na ngome ya Daniel Mgore kuwa imara kwa muda wa dakika 180.

Baraza alianza kumenyana na Gwambina FC Uwanja wa Karume kwa kushinda bao 1-0 kisha ikamaliza safari yake mbele ya Mwadui FC kwa kushinda bao 1-0 kabla ya kuondoka Mara kuifuata Simba.


Baraza amesema:”Simba ni timu kubwa ambayo inafanya vizuri katika mechi zake, lakini ikitokea timu ikaingia kichwakichwa inaweza kufungwa mabao zaidi ya yale ambayo sisi tulifungwa.


“wachezaji wangu walikwama katika kutegua makosa yao ambayo waliyatega wenyewe na nafasi ambazo walitengeneza walishindwa kutumia hilo linatufanya tuanze kujipanga upya kwa ajili ya mechi zetu zijazo.


“Bado kwa sasa ligi inaanza tuna nafasi ya kufanya vizuri hakuna haja ya kukata tamaa imani yangu ipo kwa wachezaji na nguvu ya kufanya vizuri ipo,” amesema.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *