Posted By Posted On

CHAMA AMPANDISHA MZUKA KOCHA SVEN

NA JESCA NANGAWE KOCHA mkuu wa Simba, Sven Vanderbroeck, kwasasa humwambii lolote kuhusu kiungo anayefanya vema ndani ya kikosi chake, Clatous Chama au maarufu kama Mwamba wa Lusaka. Sven ameweka wazi kwamba kiungo huyo ana faida nyingi ndani ya kikosi chake licha ya uwezo wake mkubwa uwanjani. Alisema moja ya faida yake ni aina ya
The post CHAMA AMPANDISHA MZUKA KOCHA SVEN appeared first on Gazeti la Dimba.,

NA JESCA NANGAWE

KOCHA mkuu wa Simba, Sven Vanderbroeck, kwasasa humwambii lolote kuhusu kiungo anayefanya vema ndani ya kikosi chake, Clatous Chama au maarufu kama Mwamba wa Lusaka.

Sven ameweka wazi kwamba kiungo huyo ana faida nyingi ndani ya kikosi chake licha ya uwezo wake mkubwa uwanjani.

Alisema moja ya faida yake ni aina ya uchezaji maana jinsi anavyojituma kiasi cha kuwawafanya wachezaji wenzake kutobweteka na badala yake kutamani kufikia kiwango chake.

“Chama amekuwa akiwaongezea hamasa wenzake katika mazoezi na hata katika mechi,” alisema Sven.

Pia aliongeza kwamba ndani ya kikosi cha Simba, Chama amekuwa na sifa ya kusoma mchezo na kuelekeza wenzake pindi yanapohitajika mabadiliko ya haraka.

Kutokana na sifa hizo, Sven ameutaka uongozi wa Simba kumthamini mchezaji huyo na kumpa nafasi anayostahili ili aweze kuendelea kuisaidia klabu hiyo.

Katika mechi dhidi ya Biashara United, Chama alipachika mabao mawili katika ushindi wa 4-0 iliyopata timu yake na kuiongezea pointi tatu muhimu.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara licha ya kubanwa mbavu na Mtibwa Sugar katika mchezo wake wa pili ikipata sare ya bao 1-1, ushindi wa juzi umeisogeza nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi ikicheza mechi tatu, imeshinda mbili, sare moja na kujikusanyia pointi saba.

The post CHAMA AMPANDISHA MZUKA KOCHA SVEN appeared first on Gazeti la Dimba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *