Posted By Posted On

DAVID MOYES, MENEJA WA WEST HAM UNITED AKUTWA NA CORONA

KOCHA Mkuu wa West Ham, David Moyes amekutwa na Virusi vya Corona pamoja na wachezaji wake wawili ambao ni Issa Diop na Josh Cullen.West Ham ilipokea majibu hayo muda mfupi kabla ya kuanza kwa raundi ya tatu ya mchezo wao wa Carabao Cup dhidi ya Hull uliochezwa Jana, Septemba 22 Uwanja wa London.Mchezo huo West Ham ilishinda kwa mabao 5-1 ambapo watupiaji walikuwa ni  Robert Snodgrass dk 18, Sebastian Haller 45,90+1 na Andry Yarmolenko 56,(p) na 90 lile la Hull City lilipachikwa na Mallik Wilks dk 70.Taarifa kamili iliyotolewa na uongozi wa West Ham umethibitisha kwa kusema kuwa wachezaji hao pamoja na meneja wa timu hiyo wamekutwa na Virusi vya Corona kwa sasa wapo kwenye uangalizi. “West Ham United inathibitisha kwamba David Moyes, Issa Diop na Josh Cullen wamekutwa na Covid -19. Tunawawaombea warejee kwenye ubora wao na tutafuata taratibu zilizowekwa na Ligi Kuu England kwa ajili ya kujali afya zao na zetu pia.”Kwenye mechi hiyo kocha msaidizi Alan Irvine alichukua majukumu ya kukiongoza kikosi hicho.,


KOCHA Mkuu wa West Ham, David Moyes amekutwa na Virusi vya Corona pamoja na wachezaji wake wawili ambao ni Issa Diop na Josh Cullen.

West Ham ilipokea majibu hayo muda mfupi kabla ya kuanza kwa raundi ya tatu ya mchezo wao wa Carabao Cup dhidi ya Hull uliochezwa Jana, Septemba 22 Uwanja wa London.

Mchezo huo West Ham ilishinda kwa mabao 5-1 ambapo watupiaji walikuwa ni  Robert Snodgrass dk 18, Sebastian Haller 45,90+1 na Andry Yarmolenko 56,(p) na 90 lile la Hull City lilipachikwa na Mallik Wilks dk 70.

Taarifa kamili iliyotolewa na uongozi wa West Ham umethibitisha kwa kusema kuwa wachezaji hao pamoja na meneja wa timu hiyo wamekutwa na Virusi vya Corona kwa sasa wapo kwenye uangalizi.

 “West Ham United inathibitisha kwamba David Moyes, Issa Diop na Josh Cullen wamekutwa na Covid -19. Tunawawaombea warejee kwenye ubora wao na tutafuata taratibu zilizowekwa na Ligi Kuu England kwa ajili ya kujali afya zao na zetu pia.”

Kwenye mechi hiyo kocha msaidizi Alan Irvine alichukua majukumu ya kukiongoza kikosi hicho.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *