Posted By Posted On

IKIMALIZA HILI TU YANGA HAISHIKIKI

NA EZEKIEL TENDWA HUENDA kauli hii isiwafurahishe kabisa mashabiki wa upande wa pili baada ya mchambuzi maarufu nchini, Mwalimu Alex Kashasha kuweka wazi kwamba Yanga itanoga ile mbaya. Licha ya kwamba katika michezo yake mitatu, Yanga hawakupata ushindi mkubwa, Mwalimu Kashasha amesema kwamba gari lao likiwaka hakuna atakayeweza kulizuia. Katika michezo hiyo mitatu ambayo Yanga
The post IKIMALIZA HILI TU YANGA HAISHIKIKI appeared first on Gazeti la Dimba.,

NA EZEKIEL TENDWA

HUENDA kauli hii isiwafurahishe kabisa mashabiki wa upande wa pili baada ya mchambuzi maarufu nchini, Mwalimu Alex Kashasha kuweka wazi kwamba Yanga itanoga ile mbaya.

Licha ya kwamba katika michezo yake mitatu, Yanga hawakupata ushindi mkubwa, Mwalimu Kashasha amesema kwamba gari lao likiwaka hakuna atakayeweza kulizuia.

Katika michezo hiyo mitatu ambayo Yanga wamecheza mpaka sasa ni dhidi ya Tanzania Prisons wakitoka sare ya kufungana bao 1-1, wakashinda bao 1-0 dhidi ya Mbeya City michezo yote ikichezwa Uwanja wa Mkapa kabla ya kwenda ugenini Uwanja wa Kaitaba na kushinda tena bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar.

Mwalimu Kashasha alisema kwamba, Yanga ina kikosi kizuri sana isipokuwa wachezaji hawajazoeana na wakizoeana shughuli itakuwa pevu.

“Yanga wana kikosi kizuri sana isipokuwa hawajazoeana, binafsi nadhani wakishazoeana watakuwa moto wa kuotea mbali tofauti na msimu uliopita.

“Ukikiangalia kikosi cha msimu huu kina wachezaji wazuri tena wenye uzoefu mkubwa kama akina Mukoko Tonombe, Tuisila Kisunda, Yacouba Sogne, Michael Sarpong, Haruna Niyonzima na Feisal Salum, nadhani wakielewana vizuri mashabiki wao watafurahi.

“Kilichopo kwasasa waendelee kumpa kocha wao muda akijenge vizuri maana yeye bado ni mgeni. Akishamaliza kazi hiyo ya kuwaweka wachezaji pamoja, kitakachofuata itakuwa ni burudani ya kutosha,” alisema.

Katika hatua nyingine kikosi hicho kipo kwenye mazoezi makali kuhakikisha wanawatoa nishai Mtibwa Sugar, mchezo utakaochezwa mwishoni mwa wiki hii Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, ameliambia DIMBA Jumatano kwamba kikosi chao kipo kwenye maandalizi kabambe huku lengo lao likiwa ni kuondoka na pointi zote tatu dhidi ya Wakata Miwa hao.

“Sisi tupo kamili, maandalizi yanakwenda vizuri na muda wowote kuanzia Ijumaa tutawafuata Mtibwa Sugar. Tunajua kwamba mchezo utakuwa mgumu lakini tumejiandaa vizuri kufanya kama kile tulichokifanya dhidi ya Kagera Sugar,” alisema.

Katika mchezo wao huo dhidi ya Kagera Sugar, Yanga walishinda bao 1-0 lililofungwa na Mukoko Tonombe na wanataka kuifanyia tena umafia Mtibwa Sugar.

 

The post IKIMALIZA HILI TU YANGA HAISHIKIKI appeared first on Gazeti la Dimba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *