Posted By Posted On

ISHU YA NIDHAMU YA MORRISON NDANI YA SIMBA IPO HIVI

 MENEJA Mkuu wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa hapati usumbufu wowote kutoka kwa kiungo mshambuliaji wake mpya Mghana, Bernard Morrison. Mghana huyo akiwa anaichezea Yanga inasemekana alikuwa akiwafanyia vioja na usumbufu uongozi wa timu hiyo kabla ya kujiunga na Simba kwenye msimu huu. Kati ya vioja na usumbufu ambao aliwahi kufanya akiwa na Yanga ni kuondoka kambini bila ya ruhusa kutoka kwa uongozi wakati timu hiyo ikiwa kwenye hoteli moja Mikocheni jijini Dar es Salaam. Rweyemamu amesema kuwa amefurahishwa na nidhamu kubwa anayoendelea nayo Morrison tangu ajiunge na timu hiyo kwenye msimu huu.Rweyemamu amesema kiungo wake huyo anaishi vizuri na ushirikiano mzuri kutoka kwa wachezaji wenzake, benchi la ufundi na viongozi wakati wakiwa kambini. “Morrison mbona yupo freshi hana tatizo na mtu, anaishi vizuri na wachezaji katika maisha ya tofauti nje na ndani ya uwanja, hivyo kwangu najisikia furaha. “Tangu Morrison alipojiunga na Simba hakuwahi kuleta usumbufu wowote zaidi ya kutoa ushirikiano kwa wachezaji wenzake kwa kila jambo linalotokea ndani na nje ya kambi. “Morrison ni mcheshi anayependa kujichanganya na wachezaji wenzake zaidi hajawahi kuleta usumbufu wowote ndani wala nje ya kambi na kwangu ana nidhamu ya hali ya juu,” amesema Rweyemamu.,


 MENEJA Mkuu wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa hapati usumbufu wowote kutoka kwa kiungo mshambuliaji wake mpya Mghana, Bernard Morrison.

 

Mghana huyo akiwa anaichezea Yanga inasemekana alikuwa akiwafanyia vioja na usumbufu uongozi wa timu hiyo kabla ya kujiunga na Simba kwenye msimu huu.

 

Kati ya vioja na usumbufu ambao aliwahi kufanya akiwa na Yanga ni kuondoka kambini bila ya ruhusa kutoka kwa uongozi wakati timu hiyo ikiwa kwenye hoteli moja Mikocheni jijini Dar es Salaam.

 

Rweyemamu amesema kuwa amefurahishwa na nidhamu kubwa anayoendelea nayo Morrison tangu ajiunge na timu hiyo kwenye msimu huu.


Rweyemamu amesema kiungo wake huyo anaishi vizuri na ushirikiano mzuri kutoka kwa wachezaji wenzake, benchi la ufundi na viongozi wakati wakiwa kambini.

 

“Morrison mbona yupo freshi hana tatizo na mtu, anaishi vizuri na wachezaji katika maisha ya tofauti nje na ndani ya uwanja, hivyo kwangu najisikia furaha.

 

“Tangu Morrison alipojiunga na Simba hakuwahi kuleta usumbufu wowote zaidi ya kutoa ushirikiano kwa wachezaji wenzake kwa kila jambo linalotokea ndani na nje ya kambi.

 

“Morrison ni mcheshi anayependa kujichanganya na wachezaji wenzake zaidi hajawahi kuleta usumbufu wowote ndani wala nje ya kambi na kwangu ana nidhamu ya hali ya juu,” amesema Rweyemamu.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *