Posted By Posted On

KAGERA: TUNAKUJA KIVINGINE

NA NYEMO MALECELA, BUKOBA TIMU ya Kagera Sugar ambayo wiki iliyoipita ilipoteza mechi yake baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Yanga Uwanja wa Kaitaba, hatimaye imejipanga upya kurudi kivingine katika michuano ya Ligi Kuu Bara. Kufutia kipigo cha Yanga, Kagera Sugar imejikuta ikisimama katika nafasi ya 15 katika msimamo wa ligi, ikipoteza
The post KAGERA: TUNAKUJA KIVINGINE appeared first on Gazeti la Dimba.,

NA NYEMO MALECELA, BUKOBA

TIMU ya Kagera Sugar ambayo wiki iliyoipita ilipoteza mechi yake baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Yanga Uwanja wa Kaitaba, hatimaye imejipanga upya kurudi kivingine katika michuano ya Ligi Kuu Bara.

Kufutia kipigo cha Yanga, Kagera Sugar imejikuta ikisimama katika nafasi ya 15 katika msimamo wa ligi, ikipoteza mechi mbili na kupata sare moja.

Akizungumzia mipango yao mipya, kocha mkuu wa timu hiyo, Mecky Mexime, alisema wanatarajia kurejea kivingine katika ligi ili kuwapa raha mashabiki wao.

Alisema, baada ya matokeo mabaya dhidi ya Yanga aliwapa mapumziko wachezaji wake, huku akiwataka kutafakari jinsi ya kurudi upya na leo wanatarajia kuanza mazoezi kujiandaa na mechi yao dhidi ya KMC itakayopigwa Ijumaa Septemba 25, majira ya saa 8 alasiri katika uwanja wao wa nyumbani, Kaitaba mjini Bukoba.

The post KAGERA: TUNAKUJA KIVINGINE appeared first on Gazeti la Dimba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *