Posted By Posted On

KISINDA AMPOTEZA MORRISON MOROGORO

NA PRINCE JERRY, MOROGORO MASHABIKI wa Yanga mjini Morogoro kwa kasi ya ajabu wanahamsishana kuondoa jina la Morrison katika mabanda na vijiwe vyao na kuweka la mchezaji mpya wa timu hiyo, Tuisila Kisinda. Awali wapenzi wa Yanga mjini hapa, walikuwa na desturi ya kuweka jina la mchezaji anayewika katika klabu yao na Benard Morrison alipata
The post KISINDA AMPOTEZA MORRISON MOROGORO appeared first on Gazeti la Dimba.,

NA PRINCE JERRY, MOROGORO

MASHABIKI wa Yanga mjini Morogoro kwa kasi ya ajabu wanahamsishana kuondoa jina la Morrison katika mabanda na vijiwe vyao na kuweka la mchezaji mpya wa timu hiyo, Tuisila Kisinda.

Awali wapenzi wa Yanga mjini hapa, walikuwa na desturi ya kuweka jina la mchezaji anayewika katika klabu yao na Benard Morrison alipata nafasi kubwa wakati alipokuwa Yanga, kabla ya kuhamia Simba.

Kwa hivi sasa upepo umegeukia kwa Kisinda ambaye anatajwa kuwa ndiyo chaguo la mashabiki wa Yanga mjini Morogoro.

Winga huyo wa kushoto aliyechezea timu za Maniema na AS Vita za nchini DRC kabla ya kutua Yanga msimu huu wa 2020/21, ameandaliwa mapokezi ya heshima wakati kikosi chake kitakapotua mjini hapa kwa ajili ya kukipiga na Mtibwa Sugar Jumapili ijayo.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Mwenyekiti wa tawi la Bumu, Theo Muhinja, alisema kwasasa wanahamasisha mashabiki kwenda kwa wingi katika mchezo huo ili kuona aina ya wachezaji ambao watakuwa wakiwaweka katika kumbukumbu zao na pia kuwaandalia zawadi kila wanapocheza mechi za Ligi Kuu Bara.

“Tutakuwa na utaratibu wa kutangaza mchezaji wetu wa wiki na tutampa zawadi ili kuwapa moyo wa kuitumikia timu yetu,” alisema.

Yanga itacheza na Mtibwa Sugar katika mechi ya ligi itakayochewa Jumapili ikiwa ni nafasi yao kutafuta ushindi baada ya watani wao Simba kupata matokeo ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar.

The post KISINDA AMPOTEZA MORRISON MOROGORO appeared first on Gazeti la Dimba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *