Posted By Posted On

KOCHA COASTAL UNION ASHUSHA PRESHA MASHABIKI

 JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union amesema kuwa mashabiki wasiwe na hofu na kikosi cha Coastal Union kwa kuwa wanafanyia kazi makosa ambayo wameyafanya.Msimu wa 2020/21 kikosi hicho kimeanza kwa kuchechemea baada ya kuanza kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Namungo kisha mchezo wa pili kilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 mbele ya Azam FC na mchezo wake wa kwanza Uwanja wa Mkwakwani ilitoshana nguvu bila kufungana na Dodoma Jiji.Akizungumza na Championi Jumatano, Mgunda alisema kuwa matokeo ambayo wanayapata yana maumivu kwani ni mabaya lakini sio mwisho kwao kupambana.“Matokeo tumeyapata kwenye mechi zetu za mwanzo ni mabaya kwani hakuna anayependa kupoteza wala kupata pointi moja kwa kuwa ligi inaanza imani ya kufanya vizuri ipo hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti,” alisema Mgunda.,

 


JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union amesema kuwa mashabiki wasiwe na hofu na kikosi cha Coastal Union kwa kuwa wanafanyia kazi makosa ambayo wameyafanya.

Msimu wa 2020/21 kikosi hicho kimeanza kwa kuchechemea baada ya kuanza kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Namungo kisha mchezo wa pili kilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 mbele ya Azam FC na mchezo wake wa kwanza Uwanja wa Mkwakwani ilitoshana nguvu bila kufungana na Dodoma Jiji.

Akizungumza na Championi Jumatano, Mgunda alisema kuwa matokeo ambayo wanayapata yana maumivu kwani ni mabaya lakini sio mwisho kwao kupambana.

“Matokeo tumeyapata kwenye mechi zetu za mwanzo ni mabaya kwani hakuna anayependa kupoteza wala kupata pointi moja kwa kuwa ligi inaanza imani ya kufanya vizuri ipo hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti,” alisema Mgunda.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *