Posted By Posted On

KOCHA YANGA ATAJA TATIZO LA WACHEZAJI WAKE LILIPO

 KOCHA Mkuu wa Yanga, Mserbia, Zlatko Krmpotić amewapa majukumu mapya washambuliaji wake Michael Sarpong na Yacouba Sagne kwa kuhakikisha wanafunga bao katika kila mchezo kwa kuwa anaamini yatakuwa na msaada mkubwa kwao. Mserbia huyo ametoa kauli hiyo kufuatia timu yake kufunga mabao matatu katika mechi tatu licha ya kuwa na pointi saba katika msimamo wa ligi kuu.Krmpotić amesema kuwa ana kila sababu za kuwataka washambuliaji wake wakiwemo Michael Sarpong na Yacouba Sogne kuhakikisha wanafunga mabao katika kila mchezo ili kuweza kujiweka katika mazingira mazuri kutokana na ushindani uliopo. “Wakati mwingine matokeo ya ushindi ni mazuri kwetu kwa kuwa yanatusaidia kufikia malengo japo kuwa bado hatujafikia kwenye ubora ambao kila mmoja wetu angependa kuona tukicheza hasa kwenye kufunga mabao.“Tumekuwa na idadi ndogo ya mabao ya kufunga tangu tuanze ligi na ni tatizo ambalo tunalifanyia kazi kwa kuhakikisha washambuliaji wetu wanafunga mabao ya kutosha kutokana na nafasi ambazo zitapatikana kwa sababu kama tunaweza kushinda kwa kupata pointi tatu bila ya mabao mengi huenda ikawa shida kwetu huko mbele hivyo lazima wabadilike,” amesema Krmpotić.,

 


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mserbia, Zlatko Krmpotić amewapa majukumu mapya washambuliaji wake Michael Sarpong na Yacouba Sagne kwa kuhakikisha wanafunga bao katika kila mchezo kwa kuwa anaamini yatakuwa na msaada mkubwa kwao.

 

Mserbia huyo ametoa kauli hiyo kufuatia timu yake kufunga mabao matatu katika mechi tatu licha ya kuwa na pointi saba katika msimamo wa ligi kuu.


Krmpotić amesema kuwa ana kila sababu za kuwataka washambuliaji wake wakiwemo Michael Sarpong na Yacouba Sogne kuhakikisha wanafunga mabao katika kila mchezo ili kuweza kujiweka katika mazingira mazuri kutokana na ushindani uliopo.

 

“Wakati mwingine matokeo ya ushindi ni mazuri kwetu kwa kuwa yanatusaidia kufikia malengo japo kuwa bado hatujafikia kwenye ubora ambao kila mmoja wetu angependa kuona tukicheza hasa kwenye kufunga mabao.


“Tumekuwa na idadi ndogo ya mabao ya kufunga tangu tuanze ligi na ni tatizo ambalo tunalifanyia kazi kwa kuhakikisha washambuliaji wetu wanafunga mabao ya kutosha kutokana na nafasi ambazo zitapatikana kwa sababu kama tunaweza kushinda kwa kupata pointi tatu bila ya mabao mengi huenda ikawa shida kwetu huko mbele hivyo lazima wabadilike,” amesema Krmpotić.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *