Posted By Posted On

SABABU ITAKAYOMCHOMOA CHAMA SIMBA HII HAPA

 KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amependezwa na ufundi wa kiungo wake Clatous Chama huku akibainisha kuwa ni ngumu kwa kiungo huyo kubakia klabuni hapo.Chama ndiye anashikilia Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo aliitwaa msimu uliopita baada ya kuonyesha makali. Amekuwa ndiye mchezaji mahiri zaidi kwenye kikosi cha Simba kuanzia alipojiunga nacho akitokea Power Dynamos ya nchini Zambia.Sven ambaye amekuwa ni mtu mwenye msimamo mkali, amesema ni ngumu kumbakiza staa huyo Msimbazi kwa sababu ya kiwango anachokionyesha lakini pia mkataba wake unamalizika mwakani wakati ligi itakapomalizika. Chama alijiunga na kikosi cha Simba mwaka 2018, ambapo mkataba wake utaisha Juni mwakani na kumpa uhuru wa kusajiliwa na timu nyingine. Sven amesema: “Ni maamuzi yake mwenyewe kuendelea kubaki Simba kwa mwaka huu wa mwisho wa mkataba na kila mchezaji anaweza kufanya atakachoamua.“Ningependa aendelee kubaki Simba lakini akiendelea na kiwango hiki itakuwa ngumu kumbakisha kwenye timu hii.“Tusubiri tuone, sijui nini kinaendelea akilini mwa Chama au bodi, lakini akiendelea hivi mpaka mwisho wa mkataba nitakuwa na furaha sana kwa kuwa ni mchezaji mahiri. “Uamuzi kwenye hali ya kiuchumi ya soka ilivyo sasa hivi, haupo kwa Chama mwenyewe kwa kuwa mchezo huu sasa ni biashara, hivyo tusubiri tuone nini kitatokea,” alisema kocha huyo baada ya mechi dhidi ya Biashara United ambayo kiungo huyo alifunga mabao mawili na kutoa pasi moja ya bao. Simba iliwapiga Biashara United kichapo cha mabao 4-0 na kufikisha pointi saba baada ya mechi tatu walizocheza msimu huu.,

 


KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amependezwa na ufundi wa kiungo wake Clatous Chama huku akibainisha kuwa ni ngumu kwa kiungo huyo kubakia klabuni hapo.

Chama ndiye anashikilia Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo aliitwaa msimu uliopita baada ya kuonyesha makali.

 

Amekuwa ndiye mchezaji mahiri zaidi kwenye kikosi cha Simba kuanzia alipojiunga nacho akitokea Power Dynamos ya nchini Zambia.


Sven ambaye amekuwa ni mtu mwenye msimamo mkali, amesema ni ngumu kumbakiza staa huyo Msimbazi kwa sababu ya kiwango anachokionyesha lakini pia mkataba wake unamalizika mwakani wakati ligi itakapomalizika.

 

Chama alijiunga na kikosi cha Simba mwaka 2018, ambapo mkataba wake utaisha Juni mwakani na kumpa uhuru wa kusajiliwa na timu nyingine.

 

Sven amesema: “Ni maamuzi yake mwenyewe kuendelea kubaki Simba kwa mwaka huu wa mwisho wa mkataba na kila mchezaji anaweza kufanya atakachoamua.


“Ningependa aendelee kubaki Simba lakini akiendelea na kiwango hiki itakuwa ngumu kumbakisha kwenye timu hii.


“Tusubiri tuone, sijui nini kinaendelea akilini mwa Chama au bodi, lakini akiendelea hivi mpaka mwisho wa mkataba nitakuwa na furaha sana kwa kuwa ni mchezaji mahiri.

 

“Uamuzi kwenye hali ya kiuchumi ya soka ilivyo sasa hivi, haupo kwa Chama mwenyewe kwa kuwa mchezo huu sasa ni biashara, hivyo tusubiri tuone nini kitatokea,” alisema kocha huyo baada ya mechi dhidi ya Biashara United ambayo kiungo huyo alifunga mabao mawili na kutoa pasi moja ya bao.

 

Simba iliwapiga Biashara United kichapo cha mabao 4-0 na kufikisha pointi saba baada ya mechi tatu walizocheza msimu huu.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *