Posted By Posted On

SIMBA SC YAJIGAMBA KUIKERA GWAMBINA

NA EZEKIEL TENDWA SI unakumbuka namna Simba walivyowakera Biashara United pale kwa Mkapa mwishoni mwa wiki iliyopita? Sasa Wekundu hao wa Msimbazi wamesema hao Gwambina ndio watatafuta pa kutokea. Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, waliwashushia kipigo cha mbwa mwizi Biashara United cha mabao 4-0 mchezo uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita
The post SIMBA SC YAJIGAMBA KUIKERA GWAMBINA appeared first on Gazeti la Dimba.,

NA EZEKIEL TENDWA

SI unakumbuka namna Simba walivyowakera Biashara United pale kwa Mkapa mwishoni mwa wiki iliyopita? Sasa Wekundu hao wa Msimbazi wamesema hao Gwambina ndio watatafuta pa kutokea.

Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, waliwashushia kipigo cha mbwa mwizi Biashara United cha mabao 4-0 mchezo uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita na sasa wanawasubiri Gwambina Jumamosi ijayo.

Wekundu hao wa Msimbazi ndio watakaokuwa wenyeji wa mchezo huo utakaochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam ambapo wametamba kwamba wamejiandaa kuwakera vilivyo wageni wao hao.

Katika mchezo wao dhidi ya Biashara United, Simba sio tu walipata ushindi huo wa mabao 4-0, bali walionyesha soka la kuvutia huku wakitamba kwamba watakapokutana na Gwambina ndiyo watazidi kuwapa utamu mashabiki wao.

Kocha mkuu wa kikosi hicho, Sven Vandenbroeck, alisema kwamba lengo lao ni kuhakikisha wanatetea ubingwa wao hivyo iwe jua au mvua wanazitaka pointi tatu dhidi ya Gwambina.

“Mchezo wetu uliopita (dhidi ya Biashara United) kila mchezaji alijituma sana. Kwa ujumla timu ilicheza vizuri na kuwafanya mashabiki kuondoka uwanjani wakiwa na furaha.

“Mwishoni mwa wiki hii (Jumamosi) tutakuwa tena uwanja wetu wa nyumbani kuwakaribisha Gwambina, najua utakuwa mchezo mgumu lakini tumejiandaa kuwapa furaha mashabiki wetu.

“Sisi kama Simba hatuidharau timu yoyote. Tutaingia kwenye mchezo huo kwa lengo hilo hilo moja la kushinda lakini pia tukionyesha mchezo mzuri, tunaendelea kuwaomba mashabiki wetu wazidi kutupa sapoti,” alisema.

Katika mchezo uliopita, mabao ya Simba yalifungwa na Clatous Chama aliyepachika mawili huku mengine yalifungwa na Meddie Kagere pamoja na Chris Mugalu.

Kikosi hicho cha Simba jana kilicheza tena mchezo wa kirafiki dhidi ya African Lyon Uwanja wa Chamaz ikiwa ni maandalizi ya kuhakikisha Gwambina wanalazwa na viatu.

Mpaka sasa Simba wameshacheza michezo mitatu wakianza dhidi ya Ihefu FC ugenini ambapo walishinda jumla ya mabao 2-1 yaliyofungwa na John Bocco pamoja na Mzamiru Yassin huku lile la Ihefu likifungwa na Omary Mponda.

Mchezo uliofuata walicheza dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro na timu hizo kutoka sare ya kufungana bao 1-1, lile la Simba likifungwa na Mzamiru Yassin.

Mwishoni mwa wiki iliyopita Simba ndipo wakaishushia kipigo cha mbwa koko, Biashara United, cha mabao 4-0 mabao ya Simba yakifungwa na Chama mawili, Kagere na Mugalu kila mmoja akifunga moja.

The post SIMBA SC YAJIGAMBA KUIKERA GWAMBINA appeared first on Gazeti la Dimba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *