Posted By Posted On

YANGA NA SIMBA ZIMEPOTEZANA BONGO JUMLAJUMLA

 SIKU 25 zimebaki kabla ya miamba ya soka nchini Tanzania, Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Zlatko Krmpotic na Simba  inayonolewa na Sven Vandenbroeck kukutana Uwanja wa Mkapa kusaka pointi tatu muhimu ambapo zitakutana Oktoba 18.Zote kwa sasa ndani ya ligi zikiwa zimecheza jumla ya mechi tatu ambazo ni dakika 270, Simba imeonekana kuipoteza mazima Yanga kwa upande wa safu ya ushambuliaji huku Yanga ikiwapoteza Simba kwenye safu ya ulinzi.Yanga imefungwa bao moja pekee ndani ya dakika 270 jambo linaloonesha kwamba safu yao inayoongozwa na Lamine Moro pamoja na Bakari Mwamnyeto imeanza kujibu na kuipoteza ile ya Simba inayoongozwa na Joash Onyango pamoja na Pascal Wawa ambayo imeruhusu kufungwa mabao mawili.Kwa upande wa safu ya ushambuliaji, Simba imefunga mabao saba huku watupiaji wakiwa ni Mzamiru Yassin, Clatous Chama hawa wametupia mabao mawili,Chris Mugalu, John Bocco na Meddie Kagere wametupia bao mojamoja.Matokeo ya Simba yalikuwa namna hii:- Ihefu 1-2 Simba Uwanja wa Sokoine, Mtibwa Sugar 1-1 Simba, Uwanja wa Jamhuri na Simba 4-0 Biashara United Uwanja wa Mkapa.Yanga imefunga mabao matatu ambapo wafungaji wa Yanga ni Michael Sarpong, Lamine Moro na Tuisila Kisinda. Matokeo ya Yanga kwa mechi tatu yalikuwa namna hii:-Yanga 1-1 Tanzania Prisons,Yanga 1-0 Mbeya City hizi zilipigwa Uwanja wa Mkapa na Kagera Sugar 0-1 Yanga Uwanja wa Kaitaba.,

 


SIKU 25 zimebaki kabla ya miamba ya soka nchini Tanzania, Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Zlatko Krmpotic na Simba  inayonolewa na Sven Vandenbroeck kukutana Uwanja wa Mkapa kusaka pointi tatu muhimu ambapo zitakutana Oktoba 18.

Zote kwa sasa ndani ya ligi zikiwa zimecheza jumla ya mechi tatu ambazo ni dakika 270, Simba imeonekana kuipoteza mazima Yanga kwa upande wa safu ya ushambuliaji huku Yanga ikiwapoteza Simba kwenye safu ya ulinzi.

Yanga imefungwa bao moja pekee ndani ya dakika 270 jambo linaloonesha kwamba safu yao inayoongozwa na Lamine Moro pamoja na Bakari Mwamnyeto imeanza kujibu na kuipoteza ile ya Simba inayoongozwa na Joash Onyango pamoja na Pascal Wawa ambayo imeruhusu kufungwa mabao mawili.

Kwa upande wa safu ya ushambuliaji, Simba imefunga mabao saba huku watupiaji wakiwa ni Mzamiru Yassin, Clatous Chama hawa wametupia mabao mawili,Chris Mugalu, John Bocco na Meddie Kagere wametupia bao mojamoja.

Matokeo ya Simba yalikuwa namna hii:- Ihefu 1-2 Simba Uwanja wa Sokoine, Mtibwa Sugar 1-1 Simba, Uwanja wa Jamhuri na Simba 4-0 Biashara United Uwanja wa Mkapa.

Yanga imefunga mabao matatu ambapo wafungaji wa Yanga ni Michael Sarpong, Lamine Moro na Tuisila Kisinda. Matokeo ya Yanga kwa mechi tatu yalikuwa namna hii:-Yanga 1-1 Tanzania Prisons,Yanga 1-0 Mbeya City hizi zilipigwa Uwanja wa Mkapa na Kagera Sugar 0-1 Yanga Uwanja wa Kaitaba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *