Posted By Posted On

KOCHA ARSENAL ATAKA KILA MCHEZAJI KUFUNGA

 MIKEL Arteta, Kocha Mkuu wa Arsenal amewataka wachezaji wake kumsaidia suala la ufungaji mabao straika wao namba moja, Pierre-Emerick Aubameyang.Kocha huyo alikiongoza kikosi chake kushinda mbele ya West Ham 2-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu England Jumamosi iliyopita, huku watupiaji wakiwa ni Alexandre Lacazette na Eddie Nketiah.Arteta amewataka wachezaji wahakikishe kwamba wanamiliki mpira huku kila mmoja akiwa na uwezo wa kufunga ili kuwafanya kurudi kwenye ubora wa kuhesabika kama moja ya timu matata Ligi Kuu England.“Tunahitaji kushiriki pamoja suala la kufunga mabao.Nilishawaeleza hilo. Tunahitaji kufunga kama timu iwapo tunataka kuchuana na timu kubwa kwenye ligi. Tukitegemea mchezaji mmoja hatutaweza.“Hivyo, wote ni lazima wawajibike na hilo litawahusu wachezaji wa nafasi zote ili kuweza kufikia malengo.”,

 


MIKEL Arteta, Kocha Mkuu wa Arsenal amewataka wachezaji wake kumsaidia suala la ufungaji mabao straika wao namba moja, Pierre-Emerick Aubameyang.


Kocha huyo alikiongoza kikosi chake kushinda mbele ya West Ham 2-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu England Jumamosi iliyopita, huku watupiaji wakiwa ni Alexandre Lacazette na Eddie Nketiah.

Arteta amewataka wachezaji wahakikishe kwamba wanamiliki mpira huku kila mmoja akiwa na uwezo wa kufunga ili kuwafanya kurudi kwenye ubora wa kuhesabika kama moja ya timu matata Ligi Kuu England.

“Tunahitaji kushiriki pamoja suala la kufunga mabao.
Nilishawaeleza hilo. Tunahitaji kufunga kama timu iwapo tunataka kuchuana na timu kubwa kwenye ligi. Tukitegemea mchezaji mmoja hatutaweza.

“Hivyo, wote ni lazima wawajibike na hilo litawahusu wachezaji wa nafasi zote ili kuweza kufikia malengo.”,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *