Posted By Posted On

LUIS SUAREZ MALI YA ATLETICO MADRID

 BARCELONA wamekubali kumwachilia mshambuliaji wake, Luis Suarez, ambaye ni raia wa Uruguay ajiunge na washindani wakuu katika Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga), Atletico Madrid. Suarez amekaa Camp Nou kwa miaka sita, hayupo kwenye mipango ya Kocha Ronald Koeman. Miamba hao wa soka ya Uhispania walikuwa radhi kumwachilia Suarez kujiunga na kikosi chochote bila ada ilimradi klabu ambayo angejiunga nayo si ya La Liga. Suarez alikubali kupunguziwa mshahara ili kuingia katika usajili rasmi wa Atletico baada ya uhamisho wake kwenda Juventus ya Italia kugonga mwamba kwa sababu ya changamoto za kutafuta pasipoti na kibali cha kufanyia kazi Italia. Rais wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu, alizuia uhamisho wa Suarez hadi Atletico kwa sababu hakutaka nyota huyo auzwe kwa kikosi ambacho ni washindani wao wakuu kwenye Ligi. Hata hivyo, baada ya kukutana na wawakilishi wa Suarez, Barcelona waliafikiana nao baada ya mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool kufichua mipango ya kuanika kwenye vyombo vya habari jinsi “anavyohangaishwa” na Barcelona. Suarez ataaga leo katika mkutano wake na waandishi wa habari, kabla ya kujiunga na Atletico Madrid. Barcelona imethibitisha kuwa mshambuliaji huyo raia wa Uruguay ataondoka baada ya mkutano huo. Atletico kwa sasa wameweka mezani kiasi cha dola milioni 7, sawa na Tsh bilioni 16.24 kwa ajili ya huduma za Suarez mwenye umri wa miaka 33. Hata hivyo, fedha hizo huenda zikaongezeka kutegemea jinsi Suarez atakavyowajibishwa na Atletico na iwapo ataongoza kikosi hicho cha kocha Diego Simeone kupiga hatua zaidi kwenye soka ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA). Uhamisho wa Suarez unatamatisha kipindi cha miaka sita kambini mwa Barcelona ambao amewafungia jumla ya mabao 198 kwenye mechi 283. Katika enzi za ubora wake, Suarez alishirikiana vilivyo na Lionel Messi na Neymar muungano wao almaarufu MSN ukawa tishio zaidi kwa mabeki wa kikosi chochote duniani. Suarez alijiunga na Barcelona 2014 baada ya kuagana na Liverpool kwa  Sh10.3 bilioni. Tangu wakati huo, ametwaa na Barcelona mataji manne ya La Liga, manne ya Copa del Rey, moja la UEFA na jingine la Kombe la Dunia kwa Klabu mnamo 2015.,


 BARCELONA wamekubali kumwachilia mshambuliaji wake, Luis Suarez, ambaye ni raia wa Uruguay ajiunge na washindani wakuu katika Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga), Atletico Madrid.

 

Suarez amekaa Camp Nou kwa miaka sita, hayupo kwenye mipango ya Kocha Ronald Koeman. Miamba hao wa soka ya Uhispania walikuwa radhi kumwachilia Suarez kujiunga na kikosi chochote bila ada ilimradi klabu ambayo angejiunga nayo si ya La Liga.

 

Suarez alikubali kupunguziwa mshahara ili kuingia katika usajili rasmi wa Atletico baada ya uhamisho wake kwenda Juventus ya Italia kugonga mwamba kwa sababu ya changamoto za kutafuta pasipoti na kibali cha kufanyia kazi Italia.

 

Rais wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu, alizuia uhamisho wa Suarez hadi Atletico kwa sababu hakutaka nyota huyo auzwe kwa kikosi ambacho ni washindani wao wakuu kwenye Ligi.

 

Hata hivyo, baada ya kukutana na wawakilishi wa Suarez, Barcelona waliafikiana nao baada ya mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool kufichua mipango ya kuanika kwenye vyombo vya habari jinsi “anavyohangaishwa” na Barcelona.

 

Suarez ataaga leo katika mkutano wake na waandishi wa habari, kabla ya kujiunga na Atletico Madrid. Barcelona imethibitisha kuwa mshambuliaji huyo raia wa Uruguay ataondoka baada ya mkutano huo.

 

Atletico kwa sasa wameweka mezani kiasi cha dola milioni 7, sawa na Tsh bilioni 16.24 kwa ajili ya huduma za Suarez mwenye umri wa miaka 33.

 

Hata hivyo, fedha hizo huenda zikaongezeka kutegemea jinsi Suarez atakavyowajibishwa na Atletico na iwapo ataongoza kikosi hicho cha kocha Diego Simeone kupiga hatua zaidi kwenye soka ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA).

 

Uhamisho wa Suarez unatamatisha kipindi cha miaka sita kambini mwa Barcelona ambao amewafungia jumla ya mabao 198 kwenye mechi 283. Katika enzi za ubora wake, Suarez alishirikiana vilivyo na Lionel Messi na Neymar muungano wao almaarufu MSN ukawa tishio zaidi kwa mabeki wa kikosi chochote duniani.

 

Suarez alijiunga na Barcelona 2014 baada ya kuagana na Liverpool kwa  Sh10.3 bilioni. Tangu wakati huo, ametwaa na Barcelona mataji manne ya La Liga, manne ya Copa del Rey, moja la UEFA na jingine la Kombe la Dunia kwa Klabu mnamo 2015.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *