Posted By Posted On

MKURUGENZI GSM AWAOMBA MASHABIKI KUKUBALI MABADILIKO

Msomaji wa Yanganews Blog:Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM ambao ni wadhamini wa Yanga, Hersi Said, amesema wiki ya mwanzo ya mwezi ujao wanatarajia kupokea ripoti ya mwisho ya makubaliano ya kimfumo ya timu hiyo kutoka Kampuni La Liga kupitia Klabu ya Sevilla.

Akizungumza na na chanzo chetu hapo jana, Hersi alisema mchakato huo umefika hatua nzuri na ripoti hiyo ni ya mwisho kutoka La Liga kushirikiana na klabu hiyo ambayo wanatarajia kukabidhiwa wiki ya mwanzo ya mwezi ujao (Oktoba), mwaka huu.

Alisema baada ya hatua ya kwanza ya makabidhiano, watapata utaalamu wa ndani, na kisha watautoa nje kwa kushirikisha matawi yote ya Yanga nchini nzima.

“Baada ya kupata utaalamu huo katika matawi yote ya Yanga kuelimisha na kupata ushauri wa wanachama kutokana na ripoti hiyo baadaye itapelekewa katika mkutano mkuu kupata ridhaa ya wanachama wote.

“Niwaombe mashabiki na wanachama wa Yanga, kuunga mabadiliko hayo ya kimfumo kwa sababu baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo tutawashikirisha wanchama wetu kabla ya kupeleka katika mkutano mkuu,” alisema Hersi.

Alisema pia mashabiki wajitokeze kwa wingi kusapoti timu yao ikiwa ni pamoja na kununua jezi halali na kujitokeza kwa wingi katika viwanja inapocheza timu yao

Bonyeza picha chini, kubali mabadiliko

 

,,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *