Posted By Posted On

MWAISABULA AIPA USHAURI YANGA KUMPATA NAHODHA

Msomaji wa Yanganews Blog: Kocha wa zamani wa Yanga, Kennedy Mwaisabula amesema ili mtu awe nahodha wa timu ni lazima awe na sifa zifuatavyo, kuwa kiongozi na kusikilizwa na wenzake mwenye kuunganisha wachezaji na viongozi na kuchuja anachokiwasilisha, usupa staa ndani ya timu, kupata nafasi ya kucheza kikosini mbali na kuitumikia timu kwa muda mrefu na kujua miiko na tamaduni zake.

“Ni lazima mchezaji awe na sifa hizo, ndio maana mara nyingi manahodha wanakuwa na mastaa wa timu, yaani wenye ushawishi na kusikilizwa, pia mwenye nafasi kikosini, kwangu ningetakiwa kuteua mmoja, basi Niyonzima angefaa zaidi, ila Kocha Zlatko ndiye mwenye uamuzi wa mwisho,” alisema Mwaisabula.

,,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *