Posted By Posted On

NAHODHA YANGA KUTANGAZWA HIVI KARIBUNI

Msomaji wa Yanganews Blog:Akizungumza na chanzo chetu Kocha Zlatko alisema ameshapata akili ya nani atakuwa nahodha wa timu hiyo katika kipindi cha wiki tatu alichokaa na wachezaji wake, lakini akagoma kutaja kwa sasa akisema ni mpaka viongozi watakapoyapitisha.

“Nimekaa hapa wiki tatu sasa hilo suala la nani anakuwa nahodha nimeshapata akili ya nani namuona lakini bado nataka kwanza niongee na viongozi niwasikie nao wana mawazo gani,” alisema Zlatko.

“Unajua hii ni timu na ina utaratibu wake na inawezekana hata utamaduni wake naweza kuona huyu ni mtu sahihi, ila kumbe kule kwa viongozi nikawapa wakati mgumu, sitaki hilo litokee.”

Alisema anataka awe na nahodha atakayekubalika kwake, wachezaji wenzake na hata viongozi ambapo muhimu kwake aweze kuwaongoza kwa mfano wenzake wakiwa uwanjani.

,,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *