Posted By Posted On

SAMATTA MAZOEZINI NA KLABU YAKE MPYA, FENERBAHCE KUELEKEA MECHI NA MAHASIMU GALATASARAY KESHO


Mshambuliaji mpya wa Fenerbahce akiwa mazoezini na timu yake hiyo mpya Jijini Istanbul nchini Uturuki baada ya kujiunga nayo kwa mkopo wa mwaka mmoja kutoka Aston Villa ya England wenye kipengele cha kusajiliwa moja kwa moja kwa mkataba wa miaka mitatu mwishoni mwa msimu kwa ada ya Pauni Milioni 5.5.

Samatta anaweza kuwa sehemu ya kikosi cha Fenerbahçe kwenye mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya Uturuki dhidi ya Galatasaray kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Turk Telekom Jijini İstanbul ambao utaonyeshwa na chaneli ya ESPN inayopatikana ndani ya kisimbusi cha Azam TV. 

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *