Posted By Posted On

AJE MWINGINE!

TIMA SIKILO NA AYOUB HINJO AJE mwingine.Ndiyo kauli ya Simba baada ya jana mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara,Simba kuirarua mabao 3-0 Gwambina FC mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Huu ni ushindi wa pili mfululizo kwa Simba na baaa ya mechi iliyopita kuichakaza Biashara United 4-0 na sasa
The post AJE MWINGINE! appeared first on Gazeti la Dimba.,

TIMA SIKILO NA AYOUB HINJO

AJE mwingine.Ndiyo kauli ya Simba baada ya jana mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara,Simba kuirarua mabao 3-0 Gwambina FC mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Huu ni ushindi wa pili mfululizo kwa Simba na baaa ya mechi iliyopita kuichakaza Biashara United 4-0 na sasa wanajiandaa kwenda Dodoma kupambana na JKT Tanzania Jumapili ijayo.
Shukrani kwa mabao ya mabao yaliyowekwa kimiani na Meddie Kagere, Pascal Wawa na Chris Mugalu ambayo yameifanya Simba kujisogeza nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo baada ya kufikisha pointi 10 nyuma ya vinara Azam FC wenye alama 12.

Katika mchezo huo ulioanza kwa kasi kwa timu zote kujenga mashambulizi kwa mwenzake Gwambina ndiyo walikuwa wa kwanza kulishambulia lango la wenyeji wao dakika 9 ya mchezo.
Kama siyo uimara wa kipa Aishi Manula pengine Gwambina wangepata bao la kutangulia.

Dakika ya 12, Simba walijibu mapigo kupitia kwa kiungo wake, Clatous Chama ambaye alishindwa kuiandikia timu hiyo bao la kuongoza kabla ya kupoteza nafasi nyingine iliyookolewa na mlinda mlango wa Gwambina, Makaka ambaye alisimama imara kuokoa mchomo huo uliopigwa kwa njia ya faulo.

Kwa mara nyingine Makaka alikuwa shujaa wa Gwambina baada ya kuokoa mpira wa faulo uliopigwa na Luis Miquissone. Ilikuwa dakika ya 30.

Kadiri muda ulivyokuwa ukienda, Gwambina walianza kuzidiwa vikali na Simba ambao walikuwa moto wa kuotea mbali ambapo dakika ya 40 walipata bao la kuongoza kupitia kwa Kagere aliyefunga kwa kichwa baada ya kuunganisha kona iliyopigwa na Miquissone.

Simba walienda mapumziko wakiwa mbele kwa bao moja, lililofungwa na straika huyo raia wa Rwanda ambaye akaunti yake sasa ina mabao mawili mpaka sasa.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa Mabingwa hao mara tatu wa Ligi Kuu Tanzania Bara kupata bao la pili kupitia kwa beki Wawa aliyepiga fataki kali. Hiyo ilikuwa dakika ya 51.

Bao hilo linakuwa la kwanza msimu huu kwa beki huyo ndani ya kikosi cha Simba tangu alipojiunga na Wanamsimbazi hao mwaka 2018.

Dakika ya 90, Chris Mugalu aliifungia Simba bao la tatu na kufunga ukurasa huo kwa siku ya jana ndani ya Uwanja wa Mkapa.
Kikosi cha Simba kilichocheza ni

Aishi Manula, Shomari Kapombe
Mohammed Hussein, Paschal Wawa,Deniss Onyango, Mzamiru Yassin, Saidi Ndemla, Clatous Chama/ Jonas Mkude, Larry Bwalya/ Bernard Morrison, Luis Miquissone , Medie Kagere/Mugalu.

Kwa upande Gwambina ni Mohamed Makaka,Aron Lulambo /Hamad Nassoro , Amosi Kadikilo, Novart Lufunga, Baraka Mtuwi, Yusuph Kagoma, Japhet Mayunga/ Meshack Mwamita. Yusuf Lwenge, Paul Nonga, Jacob Massawe, Rajab Athumani

The post AJE MWINGINE! appeared first on Gazeti la Dimba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *