Posted By Posted On

ALICHOSEMA ZLATKO LUELEKEA MECHI YA LIGI KUU DHIDI MTIBWA SUGAR

Msomaji wa Yanganews Blog:Kuelekea mechi ya ligi kuu dhidi Mtibwa Sugar,Kocha mkuu wa mabingwa wa kihistoria Yanga, Zlatko Krmpotic amesisitiza kwamba kikosi cha kimeanza kuimarika zaidi kiuchezaji na wiki hii walifanya mambo mengi mazoezini ambayo anaamini yataanza kuonekana leo dhidi ya Mtibwa na mashabiki watafurahia.

Krmpotic alisema anafahamu kwamba wanakutana na timu ngumu ambayo imekuwa na rekodi nzuri wakiwa nyumbani lakini hesabu zao zitabaki palepale kuhitaji ushindi.

“Tunawaheshimu Mtibwa ni timu nzuri lakini tumejipanga vyema kuhakikisha tunapata matokeo tunayolenga kuyapata ya kushinda,” alisema Krmpotic.

“Uwanja sio mzuri sana lakini kwa mazingira yoyote tunahitaji kushinda hakuna mechi rahisi kwetu tukiwa nyumbani wala ugenini hii ni changamoto lakini Yanga inahitaji matokeo,”alisema

,,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *