Posted By Posted On

LEO PATACHIMBIKA DIMBA LA JAMHURI

Msomaji wa Yanganews Blog:Leo patachimbika dimba la Jamhuri ambako Yanga itashuka dimbani kumenyana dhidi ya Mtibwa Sugar, huo ukiwa mchezo wa ligi kuu utakaopigwa saa 10jioni.

Katika mchezo wa leo, Kocha mkuu wa Yanga, Krimpotic Zlatco amemuanzisha winga wake Carlos Guimaraes ‘Carlinho’ katika mchezo wa Ligi Kuu utakaopigwa saa 10:00 jioni katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Katika mchezo huo Zlatco amemuondoa katika kikosi cha kwanza Yacouba Sogne ambaye alianza katika mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar na nafasi yake kuchukuliwa na Carlinho.

Carlinho kwenye eneo la ushambuliaji atakuwa na Michael Sarpong ambaye kwenye mchezo uliopita alisimama na Yacouba uliomalizika Yanga wakishinda 1-0 goli likifungwa na Tonombe Mukoko.

Kocha Zlatco kwenye eneo lingine hajaweka mabadiliko mengine zaidi ya kuendelea na kikosi kile kile ambacho kilipata ushindi katika mchezo uliopita.

Eneo la kipa amesimama, Metacha Mnata, mabeki ni Kibwana Shomari, Yacine Mustapha, Lamine Moro na Bakari Mwamnyeto huku kwenye eneo la viungo ni Tonombe Mukoko, Zawadi Mauya na Feisal Salum.

Upande wa washambuliaji wakiwa ni Tuisilia Kisinda na Carlos Guimaraes ‘Carlinho’ na Michael Sarpong.

Upande wa wale walio benchi ni Faruk Shikhalo, Adeyum Saleh, Abdulaziz Makame,Deus Kaseke, Ditram Nchimbi, Haruna Niyonzima na Yacouba Sogne.

Yanga mpaka sasa wanashika nafasi ya tano wakiwa na pointi saba katika mechi tatu hivyo wanahitaji ushindi ili kupata pointi tatu ambazo zitawasogeza mpaka nafasi ya nne na kuwashusha Polisi Tanzania wenye pointi saba.

,,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *