Posted By Posted On

YANGA YAENDELEZA ‘UMWAMBA’LIGI KUU

Kikosi cha mabingwa wa kihistoria Yanga SC imeendeleza umwamba katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya leo pia kuichapa Mtibwa Sugar 1-0 Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, beki Mghana, Lamine Moro aliyeunganisha kwa mguu wa kulia kona ya chini chini ya kiungo Muangola, Carlos Carlinhos dakika ya 61.

Kikosi cha Yangs kilikuwa; Metacha Mnata, Kibwana Shomari, Yassin Mustapha, Lamine Moro, Bakari Mwamnyeto, Feisal Salum, Zawadi Mauya, Mukoko Tonombe, Michael Sarpong/Ditram Nchimbi dk85, Carlos Carlinhos/ Yacouba Sogne dk70 na Tuisila Kisinda/Haruna Niyonzima dk89.

,,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *