Posted By Posted On

ZLATKO AAHIDI USHINDI YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Katika kuelekea mchezo wa leo Septemba 27, Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri, Kocha Yanga, Zlatko aahidi ushindi Yanga.

Kocha wa Yanga, Zlatko Krmpotic anasema anafahamu mechi dhidi ya Mtibwa ni ngumu, lakini taratibu anawaona vijana wake wanaimarika na kuwa na muunganiko mzuri uwanjani.

Alisema anafahamu wanakutana na timu ngumu yenye rekodi nzuri ikiwa nyumbani, lakini hesabu zao ni kupata ushindi.

“Tunawaheshimu Mtibwa, ni timu nzuri, lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata matokeo tunayolenga ya kushinda,” alisema Krmpotic

,,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *