Posted By Posted On

Kisu amfunika vibaya Manula

NA ZAINAB IDDY

KIPA  wa timu ya Azam, David Kisu, amemfunika Aishi Manula  wa Simba kutokana na kutoruhusu bao katika michezo minne ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kisu aliyesajiliwana Klabu ya Azam msimu huu, akitokea Gor Mahia ya Kenya, amechangia timu yake kushinda michezo mitatu mfululizo.

Kipa huyo akiwa katika kikosi cha Azam, kilianza kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania, kabla ya kupata ushindi wa mabao 2-0 kutoka kwa Coastal Union, michezo yote ikichezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, jijini Dares Salaam.

Baadaye, Azam ilishinda  bao 1-0 dhidi ya Mbeya City, kabla ya kuondoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, mjini Sumbawanga, mkoani Rukwa.

Kwa upande wake,  Manula amedaka michezo minne wakiruhusu mabao mawili, wakati timu yake ya Simba ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ihefu kwenye Uwanja wa Sokoine,  jijini Mbeya, kisha sare ya bao 1-1 na Mtibwa Sugar dimba la Jamhuri, mjini Morogoro.

Baadaye, Simba waliibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Biashara United, kabla ya kuifunga  mabao 3-0 Gwambina katika michezo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Mkapa, jijini Dar es Salaam.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *