Posted By Posted On

LAMINE AENDELEZA KULETA RAHA YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Lamine Moro amezidi kuipa raha Yanga baada ya kuifungia bao moja lililoipa ushindi dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri, hapo jana.

Beki huyo amefunga bao hilo kwa shuti kali akiuganisha   kona iliyopigwa na Carlos Carlinhos dakika ya 61 na kuamsha shangwe kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Mechi hiyo ambayo ilikuwa inahitimisha mzunguko wanne wa ligi kuu haikuwa na mpira wa ufundi kutokana na uwanja kutokuwa mzuri ila mbinu za walimu za kutumia mipira ya juu zilionekana kuzaa matunda ya mashambulizi mengi kila upande

Yanga kipindi cha kwanza ilipiga mashuti matatu na wakiongoza kwa umiliki wa mpira huku wakitumia mawinga kwa ajili ya kuleta mipira katikati  ingawa haikuweza kuwaletea   faida kulingana ugumu ukuta wa Mtibwa Sugar.

Akizungumza baada ya mchezo huo, kocha msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amesema waliingia kimbinu zaidi kutokana na kufahamu mazingira ya uwanja sio rafiki

“Kocha amekaa na timu siku 20, unaona kabisa timu inabadilika na inatengenezeka taratibu. Kuna muda tutaanza kutoa dozi goli 10 , 8 siku chache zijazo

“Kumtumia Carlinho pembeni ilikuwa mbinu ya mchezo, ni mchezaji mzuri ambaye mipira yake huwa na madhara kwa wapinzani, hivyo tulilazimika kumweka pembeni ili apate nafasi ya kucheza bila kuzongwa

“Mapungufu ya leo unaenda kuyafanyia kazi na tutarudi tukiwa bora zaidi mchezo ujao dhidi ya Coastal Union,” amesema

,,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *