Posted By Posted On

Wachezaji Gwambina wapewa muda

NA ZAINAB IDDY

KOCHA wa timu wa  Gwambina, Fulgence Novatus, amesema amewapa muda wachezaji wake  ili aweze kutathimini kiwango cha kila mmoja.

Gwambina inayoshiriki kwa mara ya kwanza ligi hiyo,  haijashinda katika michezo minne iliyochezwa,  huku Novatus  akitoa michezo  tisa kati ya 10 ili aweze kufanya tatathimini  ya  viwango vya wachezaji wake.

 Akizungumza na BINGWA, jijini Dar es Salaam juzi, baada ya timu yake kufungwa mabao 3-0 na Simba,  kwenye Uwanja wa Mkapa, Novatus  alisema baada ya kupoteza mchezo wa kwanza wa ligi hiyo dhidi ya Biashara United alikaa na wachezaji na kuwapa michezo 10 ya kujitathimini wenyewe.

“Kila mchezaji anajua benchi la ufundi limetoa mechi 10 za kujitathimini kabla ya kuamua akina nani tutafanya nao kazi na wengine kuachana nao katika usajili wa dirisha dogo.

“Kiuhalisia mechi 10 ni nyingi kwa timu kama itatokea tutapoteza,  lakini kwetu itatusaidia kuchagua wa kubaki nao ambao watakuja kutupa matokeo ya alama tatu,” alisema Novatus. Gwambina  walianza ligi hiyo kwa kufungwa bao 1-0 na Biashara United, kisha suluhu na Kagera Sugar, kabla ya kufungwa bao 1-0 na Ruvu Shooting na baadaye kuchapwa mabao 3-0 na  timu ya Simba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *