Zahera awapa Simba taji mapema
NA ZAINAB IDDY
BAADA ya Gwambina kufungwa mabao 3-0 na Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Mkapa, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa timu hiyo, Mwinyi Zahera, amesema Wekundu wa Msimbazi walikuwa ubora zaidi yao.
Akizungumza na BINGWA Dar es Salaam jana, Zahera alisema kikosi cha msimu huu cha Simba ni bora kuliko msimu uliopita na kinaweza kutwaa taji la nne mfululizo.
Zahera alisema tangu afanye kazi katika mpira wa Tanzania, msimu huu amekiona kikosi cha Simba kwenye kiwango bora zaidi.
“Kwa timu za Ligi Kuu hakuna iliyobora msimu huu zaidi ya Simba na kwa mashindano ya ndani wanaweza kutetea ubingwa msimu huu.
Kwa maana hii, kitaifa Simba haina mpinzani lakini kimataifa wanatakiwa kujipanga upya kwa mwakani na sio mwaka huu,” alisema Zahera.
Simba wamefanikiwa kushinda michezo mitatu, huku wakitoka sare moja, tangu ligi hiyo ilipoanza Septemba 7, mwaka huu.
,
Comments (0)