Posted By Posted On

BUMBULIA ATAJA CHANZO CHA VURUGU, VIWANJANI

Msomaji wa Yanganews Blog:Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Hassan Bumbuli ameitaka klabu ya Simba iwakemee mashabiki wake kuwa wanapokwenda uwanjani kutazama mechi za Yanga waache kutumia maneno ya kejeli na kashfa kwa mashabiki wa Yanga.

Bumbuli amesema “Simba inapaswa ikemee mashabiki wake kuwa wanapaswa kuwa wastaarabu pale wanapokwenda kutizama mechi za Yanga. Wasiingie uwanjani kwa lengo la kuwakera na kuwakejeli mashabiki wa Yanga, kejeli siku zote hazivumuliki”

“Lakini hata sisi viongozi wa hivi vilabu, tupunguze kutukana, kudhalilisha na kukera watu. Jambo hili linapandikiza chuki kwa mashabiki,” alisema Bumbuli

“Unakuta shabiki wa Simba anatamba kuwa anakwenda uwanjani kuangalia mechi za Yanga kwa lengo la kuhakikisha Yanga inafungwa, hili ni jambo la hatari kwa sababu hata mtu anapokuja nyumbani kwako na kukuambia atahakikisha hulali vizuri na familia yako huwezi kumchukulia vizuri”

Jana klabu ya Yanga ililaani matukio ya vurugu viwanjani wakilitaka Jeshi la Polisi kuchukua hatua stahiki kwa wote waliohusika. TFF, Bodi ya Ligi nao walilaani matukio hayo.

,,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *