Posted By Posted On

LAMINE MAMBO ‘BAM BAM’ YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Beki wa Yanga SC, Lamine Moro ameongeza mkabata wa miaka miwili kuendelea kuitumikia klabu hiyo hadi 2023.

Awali mkataba wa Lamine ulikuwa ukitarajiwa kumalizika Agosti mwakani hivyo mabosi wa klabu hiyo wakaona kuna umuhimu wa kumpiga kitanzi mapema cha miaka mingine miwili ili aiweze kuchukuliwa na timu nyingine.

Lamine ambaye ni raia wa Ghana amekuwa mmoja wa wachezaji muhimu kwenye kikosi cha Yanga hasa katika idara ya ulinzi  ambayo amekuwa akicheza sambambana   na Bakari Mwanyeto kama mabeki wa kati.

Tangu arejee kutoka katika majeruhi, Lamine ambaye aliukosa mchezo wa kwanza wa ligi msimu huu dhidi ya Tanzania Prisons, ameisaidia Yanga kupata pointi tisa kwenye michezo mitatu iliyopita ya Ligi Kuu Bara.

Beki huyo ambaye aliipa pointi tatu muhimu timu yake katika michezo miwili baada ya kuifungia mabao, dhidi ya Mbeya City iliposhinda bao 1-0 na dhidi ya  Mtibwa Sugar iliposhinda bao 1-0 huku pia akiingoza kuifunga Kagera Sugar bao 1-0.

Mbali na kuiongoza Yanga kutoruhusu bao kwenye michezo hiyo  mitatu, Lamine alifunga mabao mawili muhimu ambayo  yaliifanya Yanga kuibuka na ushindi kwenye michezo miwili tofauti.

Lamine licha ya kuwa beki wa kati ndiye mchezaji anayeoongoza kwa mabao kwenye kikosi cha Yanga akiwa amefunga mabao mawili huku  akifuatiwa na Michael Sarpong na Mukoko Tonombe waliofunga bao moja moja kila mmoja.

,,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *