Posted By Posted On

Lawama, chuki, matusi, dhihaka na hata wakati mwingine kuhatarisha maisha yao kutokana na kazi zao imekuwa ni kawaida kwa waand…

Lawama, chuki, matusi, dhihaka na hata wakati mwingine kuhatarisha maisha yao kutokana na kazi zao imekuwa ni kawaida kwa waandishi wengi wa habari za michezo nchini hasa pale wanapofichua madhaifu au maovu ya hizi timu mbili kubwa nchini za Simba na Yanga, Salehe Ally na Shaffih Dauda na wandishi wa habari wengine wengi wamekuwa ni wahanga ambao wamekuwa wakishambuliwa vikali pale wanapoibua maovu ya hizi timu mapacha na wanaonekana hawana maana kabisa licha ya mchango wao mkubwa Katika mpira wa Tanzania,

Shaffih Dauda aliwahi kuingia kwenye mgoggoro mkubwa sana na klabu ya Simba, utata wa mkataba wa Singano na Simba, Ramadhani Singano alikuwa anasema kwamba mkataba wake na Simba ulikuwa umefika tamati Mwaka 2015 hivyo alikuwa huru kwenda Katika klabu ya Azam iliyokuwa ikimuhitaji na Simba wao walikuwa wanadai kataba wa Singano unaisha 2016 hivyo kwa kipindi hicho alikuwa ni mchezaji wao halali, lakini wakati hili likiendelea Shaffih Dauda aliibua uozo mwingine kuhusu maisha ya Ramadhani Singano, Shaffih Dauda ndiye aliyefichua Siri kuwa Ramadhani Singano alikuwa anaishi Gheto na kaka yake yaani ukubwa wa jina lake na maisha aliyokuwa anaishi havikuwa sawa kabisa,

mchezaji wa klabu kubwa Kama Simba kuishi maisha yale haikuwa sawa, mchezaji mwenye kipaji kikubwa Kama Singano kuishi maisha yale haikuwa sawa, mwisho wa sakata hilo Ramadhani Singano alifanikiwa kwenda Azam, Jambo hilo lilichochea chuki kubwa Kati ya mashabiki wa Simba na Dauda ijapokuwa ilimsaidia mchezaji mwenyewe lakini pia iliwasaidia Simba, Simba walianza kuwa makini na mikataba ya wachezaji wao pia walianzia hapo kuona umuhimu wa kuwajali wachezaji na kuwatengenezea mazingira mazuri ya kuishi ili wafanye kazi yao vizuri, leo Simba ni klabu ambayo wachezaji wake wanaishi vizuri Sana na wachezaji wengi Africa mashariki na Kati wanatamaini kuisha maisha Kama ya wachezaji wa Simba, hakuna ubishi hata Morisson moja ya kitu kilichomvutia Simba ukiacha maslai ni mazingira mazuri ambayo klabu ya Simba imetengeneza baada kuingia Katika mfumo wa kisasa, Simba, leo hii hakuna mchezaji wa Simba ambaye anaishi Gheto Kama alivyokuwa anaishi Ramadhani Singano, Hii yote kwasababu Kuna watu Kama Shaffih Dauda walikubali kuvaa mabomu

Ukiacha hilo sakata la Dauda na Simba, Hivi karibuni mwandishi wa habari Salehe Ally mmiliki wa Website ya Salehe Jembe na mwandishi wa habari za Michezo wa Global publishers ameonekana kuwa adui mkubwa wa mashabiki wa klabu ya Yanga kwa kuandika habari zinahusu mikataba ya wachezaji wa Yanga,

Hakuna ubishi Kumekuwa na ujanja ujanja mwingi Sana unafanyika Katika mikataba ya wachezaji ya klabu nyingi nchini hususa ni Simba na Yanga, mara nyingi mashabiki wakiaminishwa baadhi ya wachezaji wao pendwa wana mikataba kumbe hawana, wamekuwa wakiaminishwa kuwa wachezaji wao pendwa wana mikataba ya muda mrefu lakini sio kweli,

Mfano Hersi Said aliwahi kutoa taarifa kwenye vyombo vya habari kuwa wamemsainisha aliyekuwa nahodha wao Papy Tshishimbi mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu ya Yanag Jambo ambalo halikuwa la kweli,

Wakati sakata la Tshishimbi halijapoa, Salehe Ally akaibua sakata lingine la utata wa mkataba wa Bernard Morisson, Salehe alifanya mahojiano na Morisson na ikaonekana mkataba wa Morrison na Yanga ulikuwa una utata Sana, kilichoendelea kila mtu anakijua hilo sitaki kuliongelea Sana,

Salehe Ally kwa Mara nyingine tena juzi amefichua kuwa beki tegemeo wa Yanga Lamine Moro hana mkataba, alishambuliwa Sana na mashabiki wa Yanga, ikaonekana ni kibaraka wa upande wa pili, Jambo amabalo sio kweli, Mashabiki wa Yanga wakiendelea kupinga vikali wakiamini kuwa Moro ana mkataba, Wakafikia mpaka hatua ya kuanzisha kampeni ya kujiondoabkwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii,

Leo hii ukweli umebainika baada Moro kusaini mkataba mpya miaka 3 kuendelea kuitumikia klabu ya Yanga, Bila Salehe Ally kuibua hii inshu pengine Moro asingepewa mkaba mpya leo na pengine mngekuwa kwenye hatari kubwa ya kumpoteza,

Mpira wetu una madudu mengi sana, kuanzia TFF mpaka kwenye vilabu vyenu pendwa vya Simba na Yanga, Kuna ujanja ujanja mwingi sana unaendelea ambao unasababisha mpira wetu usiendelee, hawa watu ambao wameamua kuvaa mabomu na kuyaibua haya madudu ambayo yanakwamisha mpira wetu kuendelea mnatakiwa kuwashukuru na kuwatia moyo kwasababu sio wote wenye ujasiri Kama huu,

Simba kupitia sakata la Singano walijifunza kitu, na ndio maana tunaona wamekuwa makini Sana kwenye masuala ya mikataba ya wachezaji, Sakata la Singano na Simba halina tofauti na sakata la Morisson na Yanga, kwanini na nyie Yanga msijifunze kupitia sakata Morisson? Mnataka kurudia tena Moro,

Tatizo la mashabiki wetu wengi walianza kuzipenda klabu kabla ya kuupenda mpira wenyewe na ndio Sababu wengi wamekuwa na mihemko mikubwa Sana, Jambo linalopelekea washindwe kusimamia ukweli Katika Mambo mbalimbali yanayohusu klabu zao,

Ngoja niwaambie kitu kimoja, mashabiki ni nguzo muhimu sana Katika soka, Mashabiki wana nguvu sana, nguvu ya mashabiki wengi ingekuwa inatumika kukosoa na kuungana pamoja kusimamia ukweli Katika mambo mbali mbali yanahusu mpira wetu, tungekuwa tungepiga hatua sana Katika soka, badala yake wengi wamejaa mihemko, hawataki kuhusu klabu zao, hawapendi habari mbaya kuhusu klabu zao ziandikwe,

Imefika hatua ushabiki unataka uanze kutugawa, tumeanza kupigana kwasababu ya ushabiki, itakadi za usimba na Uyanga zisitugawe ikafikia hatua tukawa maadui, mpira ndio Mchezo ambao huwaunganisha watu wa itakadi tofauti, Mashabiki wa Simba na Yanga ni watani wa jadi, kiasili utani wa jadi hudumusha amani na upendo, kwanini mashabiki wa kizazi hiki tunataka kubadilisha dhana ya utani wa jadi kuwa chuki na uhasama, Tusifike huko ndugu zangu.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *