Posted By Posted On

MAYAY ATAJA KINACHOIKWAMISHA YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Mshambuliaji wa zamani wa Yanga na mchambuzi, Ally Mayay amesema tatizo la Yanga ni muda tu kuwa na timu nzuri, akisisitiza utamaduni wa soka la Yanga la kutumia mawinga bado haujabadilika.

β€œNi mabadiliko tu ya makocha yameifanya kubadilika wakati mwingine kwa kutumia viungo wengi kuliko mawinga, hivyo kujikuta wakienda katika mfumo ambao unatumiwa zaidi na watani zao, Simba wa kucheza pasi fupi fupi.

β€œHata hivyo kwa sasa kwa Yanga ilivyo kiwango si kipaumbele chao kikubwa zaidi ya ushindi kutokana na aina ya kikosi walichonacho, ambacho kina wageni wengi na hakina muunganiko, hivyo kujikuta wakipiga pasi ya kwanza ya pili wako golini,” alisema Mayay.

Mayay alisema hata kwa mawinga waliopo ndani ya kikosi hicho winga ambaye anaweza kucheza kuendana na asili ya soka la timu hiyo ni Mcongo Tuisila Kisinda kwani ana kasi kama ilivyokuwa kwa mawinga waliopita akiwemo Simon msuva.

,,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *