Posted By Posted On

TAIFA STARS KUKIPIGA OKTOBA 11

Msomaji wa Yanganews Blog:TIMU ya soka ya Taifa (Taifa Stars), itacheza mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya majirani zao Burundi (Intamba Murugamba), itakayochezwa Oktoba 11, mwaka huu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini, Dar es Salaam.

Akizungumza na chanzo chetu hapo jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo, alisema wageni wao wameshathibitisha kupokea mwaliko huo na mechi hiyo inachezwa siku inayotambulika kwenye Kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

Ndimbo alisema maandalizi ya mchezo huo yameshaanza na wachezaji watakaoingia kambini kujiandaa na mechi hiyo watajulikana Oktoba 2, mwaka huu. “Tunapenda kuwaarifu Taifa Stars itakuwa na mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi, Kocha Mkuu, Etienne Ndayiragije atatangaza kikosi kitakachopeperusha bendera ya nchi katika mchezo huo Ijumaa Oktoba 2,” Ndimbo alisema.

Taifa Stars itatumia mechi hiyo pia kujiandaa na michezo ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Qatar mwaka 2022 na Fainali za Kombe la Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zitakazochezwa mapema mwakani. Katika kikosi cha Stars, Ndayiragije anasaidiwa na makocha wazawa wawili ambao ni Juma Mgunda na Selemani Matola “Veron”.

,,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *